HOFU YATANDA AFYA YA MANDELA
Kwa
mujibu wa taarifa zilizotolewa na Ikulu ya nchi hiyo mjini Pretoria zilisema
mpaka kufikia leo jioni Mandela alikuwa amezidiwa ingawa
madaktari wanafanya kila wawezalo kuhakikisha kuwa anapata afueni, ingawa ikulu
iliwahakikishia wananchi kuwa wasiwe wasiwasi sana.
Mandela
ambye alikuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, akiwa na umri wa miaka
94, alipelekwa hospitalini mapema mwezi huu, ikiwa ni mara ya tatu kwake kulazwa
hospitalini akiugua ugonjwa wa mapafu mwaka huu.
Rais
Jacob Zuma alisema Jumapili kuwa alimzuru Mandela Hospitalini na kuzungumza na
mkewe kuhusu hali ya rais mstaafu.
Madaktari wanaomtibu Mzee Nelson Mandela walimwambia
Rais Zuma kuwa hali ya Mandela imekuwa sio nzuri kwa saa zaidi ya ishirini na
nne zilizopita na yupo mahututi.
Nje
ya hospitali alikolazwa Mandela, watu wamekuwa katika hali ya utulivu huku wanafamilia wake
wakirejea toka sehemu mbalimbali duniani. Kuta za hozpitali hiyo zimeonekana
kupambwa na kadi nyingi na maua ya
kumtakia heri, na kupona haraka Rais huyo wa zamani.
Taarifa
zaidi zina bado Mzee Mandela ameendelea kusalia hospitalini mjini Pretoria kwa
siku ya kumi na sita akitibiwa mapafu yaliyosababisha tatizo kwenye mfumo wake
wa upumuaji.
Rais
Jacob Zuma amemtembelea Mzee Mandela na pia kuzungumza na jopo la matabibu
wanaomtibu. Zuma alirejea kauli yake ya kulitaka taifa na dunia kumuombea Mzee
Mandela apate nafuu.
No comments:
Post a Comment