KAMATI YA MISS TANZANIA YATEMBELEA KAMBI YA REDD'S MISS KINONDONI 2013
Mkuu
wa Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania, Albert Makoye akiongea machache
wakati kamati hiyo ilipotembelea Kambi ya Mazoezi ya Redds Miss
Kinondoni 2013 iliyopo katika hoteli ya JB Belmont hoteli jijini Dar es Salaam. Kutoka upande wa mkuu wa Itifaki ni katibu
Bosco Majaliwa, Mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundega,
mjumbe wa kamati hiyo, Lucas Rutta wakiwa pamoja muandaaji wa mashindano
hayo Dennis Ssebo.
Mkurugenzi
wa kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundega, akiongea na warembo
wanaowania taji la Redds Miss Kinondoni 2013 mara baada ya kuwatembelea
kambini kwao na kujua wanaendeleaje. Lundenga aliwaasa washiriki hao
kuongeza bidii katika mazoezi yao ili waweze kufanya vyema katika
fainali yao.
Warembo wa Redds Miss Kinondoni wakiwa wamejipanga mara baada ya kumaliza mazoezi.
---
Kamati
ya Miss Tanzania ikiongozwa na Mkurugenzi Hashimu Lundenga imetembelea
kambi ya Redds Miss Kinondoni 2013 wanaotarajiwa kumenyana leo alhamisi
(leo) ya Juni 20 katika shindano Redd’s Miss Kinondoni Talent 2013
katika ukumbi wa Shekinah Garden, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
mratibu wa shindano hilo mara baada ya kuwakaribisha wageni, Dennis
Ssebo alisema maandalizi ya kuelekea shindano hilo yanaendelea vizuri na
kueleza mshindi atakabidhiwa zawadi zake kwenye fainali ya shindano
hilo ambalo litafanyika Juni 21 mwaka huu katika uwanja wa hoteli ya
Golden Tulip.
Alisema
kwamba shindano la mwaka huu litaandika historia mpya ya urembo kwa
wilaya ya Kinondoni maana wamejipanga na kupata sapoti ya kutosha, hivyo
mashabiki wa mashindano ya urembo wakae mkao wa kupata raha.
Mashindano
ya Redd's Miss Kinondoni yamedhaminiwa na Redd's Original, Chilly Willy
Energy Drink, Oriflame Natural Beauty Products, Kiota cha Maraha
WANTASH, Virago, Times Fm, JB Belmonte Hotel, Michuzi Media Group,
Michuzijr Blog, Mtaa Kwa Mtaa Blog, Fullshangwe Blog, HandeniKwetu Blog,
Mrokim Blog, TheHabari.com, JestinaGeorge Blog, SufianMafoto Blog,
Global Publisher, Mdimuz Blog, Lukaza Blog, MO Blog na Kajunason Blog.
No comments:
Post a Comment