*MWENYEKITI UVCCM TAIFA SADIFA JUMA HAMISI APINGA MFUMO WA SERIKALI TATU
Sadifa ameyasema hayo wakati akizungumza na
wanachama wasomi wa UVCCM kutoka katika vyuo vikuu mkoani kilimanjaro katika
hafla ya kuwaaga wasomi hao na ambapo pia ametunuku vyeti vya uanachama kwa wanafunzi
312 pamoja na kuwakabidhi kadi za uanachama wanachama wapya.
Amesema bila amani na muungano wa wananchi maendeleo
hayawezi kupatikana katika nchi ambpo aliwataka vijana kuwa mtari wa mbele
kuwaelimisha wananchi wa kawaida juu ya umuhimu wa kuenzi, kudumisha na kuimarisha
muungano wa zanzibar na Tanganyika kama
njia pekee ya kuhakikisha nchi inakuwa na amani siku zote.
Katibu wa UVCCM manispaa ya Moshi, Bwana Makwaiya akisakata Rumba muda mfupi baada ya maandamano kuwasili katika makao makuu ya CCM mkoa wa kilimanjaro |
“Vijana tuna wajibu kubwa wa kuwaenzi waliotuletea
muungano wetu wa sasa, taaluma zetu ziwe dira ya jamii katika kuenzi, kudumisha
na kuimarisha muungano wetu kwani ndio njia pekee ya kusaidia kudumisha amani
na usalama wan chi yetu, tuepuke kujiingiza katika mkumbo wa wale wanaodai nchi
haitatawalika,” amesema
Hata hivyo Sadifa amewataka vijana kutodanganyika na
vyama vinavyoeneza chuki na maandamano yasiyokuwa na msingi wowote huku
akifafanua kuwa kisheria kuandamana na haki ya msingi lakini ifuate sheria na
yassingilie haki za wengine.
Sadifa akikabidhi cheti cha unachama kwa mwanafunzi wa chuo kikuu muccobs jana, jumla ya wanavyuo 312 walipata vyeti vya uanachama wa UVCCM. |
“Chama pekee katika nchi hii ni CCM, kuna vyama
vingine vimeanzishwa ambavyo mimi binafsi naviita ‘Saccos’, hauwezi
ukajikopesha fedha kienyejienyeji kama alivyofanya Dk. Slaa! Vijana tuwe makini
na saccos hizi ambazo ajenda zao ni kukopeshana na vurugu tu,” amesema Sadifa.
Kwa upande wake mwenyekiti wa shirikisho la wanafunzi
wa vyuo vikuu wanachama wa CCM kilimanjaro, Wakati Mtulya akizungumzia
changamoto wanazokumbana nazo, alisema kumekuwa na urasimu ndani ya bodi ya
mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, ambapo mikopo imekuwa ikitolewa kwa watu
wasiostahili huku walengwa wakiendelea kutaabika.
Sadifa (aliyevaa suti) akiongoza vijana kucheza kwaito katika ukumbi wa CCM mkoa wa Kilimanjaro |
“Mikopo ni yetu, sio ruzuku, lazima tukopeshwe kwa
wakati kwani lazima tutairudisha lakini jambo la kusikitisha, bodi hii imekuwa ikitoa
mikopo kwa watoto wa masaki, huku sisi watoto wea mkulima tukiendelea
kuzungushwa na kuwekewa masharti magumu ili kupata mikopo hiyo, hili ni tatizo,”
amesema Mtulya.
No comments:
Post a Comment