EXCLUSIVE Interview na MISS YUNAR MAGICION.
Miss Yunar Magicion ni msanii wa Kitanzania anayekuja kwa
kasi katika tasnia ya Muziki hapa nchini, kwa track zake mbili alizozitoa
“Nisamehe aliyomshirikisha Ben Pol” na “Hoi aliyomshirikisha Drea” ni ushahidi tosha
kuwa Miss Yunar ni moto wa kuotea mbali, Baada ya kuliona hilo nilifanya
jitihada za kumtafuta Miss Yunar Magicion ili kufanya naye Interview, na hivi
ndivyo ilivyokuwa:
Anaclet: Mambo
vipi Miss Yunar, uko poa?
Miss Yunar: Poa
tu mkaka, mzima wewe?
Anaclet: Mi nipo
njema sana, Miss Yunar unaweza kutupa japo kwa ufupi historia yako?
Miss Yunar: About
Music or what?
Anaclet: Yes,
about music.
Miss Yunar: Eeh..
tangu mwaka 2011 mwezi wa 10 nilipomaliza Elimu yangu ya Sekondari ndipo
nilipoamua kujihusisha na Muziki, na safari yangu ya kwanza katika muziki
ilianzia katika kituo kimoja kinachofahamika kama “mkubwa na wanawe” ambapo
nilikaa mpaka mwaka jana mwezi wa 8 na ndipo nikahama na kwenda kwa “Sheddy
Clever – BURN RECORD” nikafanikiwa kutengeneza nyimbo yangu iitwayo “NISAMEHE”,
kwa Sheddy pia nilikaa kwa muda mfupi, na mpaka sasa nipo mwenyewe sina
management, na nimefanikiwa kurekodi nyimbo zingine mbili katika studio
nyingine iitwayo “NATAL RECORD” iliyoko Mburahati jijini Dar es Salaam chini ya
Producer ABBAH PROCESS..
Anaclet: Idea ya
kutunga wimbo wa Nisamehe uliomshirikisha Ben Pol uliupata wapi?
Miss Yunar: Ni
idea yangu mwenyewe.
Anaclet: Kwanini
uliamua kumshirikisha Ben Pol katika huo wimbo wako wa kwanza?
Miss Yunar: Ni
ushauri na maamuzi ya producer, alivyomaliza kuitengeneza huo wimbo akaona ni
bora ashirikishwe msanii wa kiume ambaye ni Ben Pol.
Anaclet: Miss
Yunar, wewe ni msanii unayekuja kwa kasi sana katika tasnia hii ya muziki
nchini Tanzania, je ni vikwazo gani umekuwa ukikumbana navyo?
Miss Yunar:
Vikwazo ni vingi sana ten asana, inafikia kipindi natamani hata nikate tama lakini nasema hapana coz
sanaa ni kazi yangu na ndiyo Mungu aliyonipangia so siwezi kuiacha mfano meneja
au mtu yoyote ambaye ana ufahamu vizuri njia za muziki, ukimpelekea kazi yako
kwa lengo la kutaka kusaidiwa lazima atatanguliza suala la mapenzi mbele,
nadhani hilo halina ubishi na sidhani kama kuna msanii wa kike asiyefanyiwa
hivyo na vinginevyo.
Anaclet: Na wewe
kama msanii mwenye malengo makubwa mbeleni, unakabiliana vipi na vikwazo kama
hivyo?
Miss Yunar:
Daah.. me najua nini nafanya na nini nahitaji katika maisha yangu ya muziki,
kwahiyo siwezi kukubali kufanya kitu kibaya kwasababu ya msaada wake.
Anaclet: Na
kwanini uliamua kujiita Miss Yunar?
Miss Yunar: Kwanza
kabla ya kujiita “miss Yunar”, mimi nilikuwa najiita “Yunar” ila baada ya
kufanya wimbo na Ben Pol, ukiusikiliza vizuri mwishoni Ben Pol anamalizia kwa
kutaja “Miss Yunar” ndipo kila mtu alipokuwa akiusikiliza ule wimbo lazima
aniite jina la Miss Yunar na hapo ndipo hilo jina lilipoanzia.
Anaclet: Baada ya
kutoa track zako mbili, jamii inayokuzunguka inakuchukuliaje? Coz kuna wasanii
wakishatoka wanaanza kuonyesha dharau na majivuno, hii wewe kwako lipoje?
Miss Yunar: Kwa
upande wangu mimi sipo hivyo kabisa coz sioni faida ya mimi kuwa hivyo, yaani
jamii yangu naishi nayo vizuri na bila matatizo yoyote…sina dharau wala
majivuno.!
Anaclet: Hongera
sana Miss Yunar, kuna wasii wengi sana
hapa nchini na wenye majina makubwa, unaweza kuniambia ni wasanii gani
unawakubali zaidi?
Miss Yunar: Kwa
upande wa wasanii wa kike ni LADY JAYDEE, PIPI na LINAH na kwa wasanii wa kiume
ni BEN POL, Q CHILLAH, PROFESOR J na MABESTE.
Anaclet: Nini malengo yako kimuziki baada ya miaka mitatu au mitano ijayo? Au sisi
mashabiki wako tutegemee nini kutoka kwako ?
Miss Yunar : Kwanza kabisa bado nahitaji support kutoka
kwa mashabiki, mashabiki wanisupport mimi katika muziki wangu ili kufanya
muziki wangu kusonga mbele na kufikia mpaka level za kimataifa, lakini pia
lengo langu kubwa ni Taifa limjue, limfahamu Miss Yunar ni nani na anafanya
nini katika tasnia hii ya muziki na baada ya hapo nchi nyingine zinifahamu pia
lakini kwanza nyumbani Tanzania, hayo ndo malengo yangu, lakini pia ukiacha
hilo nina lengo la kuitangaza nchi yangu kupitia kipaji changu cha muziki..
Anaclet : Unazungumziaje kuhusu gharama za kurecord nyimbo hapa nchini, je
haiwabani sana wasanii chipukizi kuweza kurecord nyimbo zao ?
Miss Yunar : Mmh.. kwa upande wangu mimi sijajua kuhusu
hilo na sina jibu kamili kwasababu unapozungumzia gharama ya kurecord
inategemea na makubaliano kati ya msanii na producer, wakati mwingine mtu
anaweza akafanya nyimbo hata free na inategemea labda producer alimkubali sana
msanii katika uimbaji na ndipo akaamua kumsaidia lakini kubwa ni makubaliano
yao tu.
Anaclet : Kwa kumalizia Miss Yunar, unaiambia nini serikali kuhusu kuwasaidia
wasanii wanaochipukia ? na unawaambia nini wapenzi na mashabiki
wako ?
Miss Yunar : Daah.. mi kwa kweli naiomba serikali
itunyooshee mkono wasanii, iwe karibu na wasanii na iwasaidie kwa hali na mali
bila kujali, na pia itambue thamani ya msanii katika nchi na lingine wasanii
wenyewe tuonyeshe umoja bila kujali huyu ni star au underground au huyu ni
Bongo fleva au Hip Hop, kwa misingi hiyo tutafika mbali, lakin kubwa na la
zaidi ni support ya mashabiki ndiyo kil akitu kwangu… kwani bila wao hakuna
Yunar.
Anaclet : Thanks Yunar for your time na kukubali kufanya interview na mimi na
hii isiwe ndiyo mwisho wa kukubali wito wangu pindi nitakapokuhitaji tena..
mimi na watanzania tupo pamoja na wewe na tutakupa support ya kutosha ili
kufikia malengo yako kimuziki and for sure mimi nimekukubali sana.
Miss Yunar : Asante sana, na mimi pia nimekukubali na
Mungu akubariki na akusimamie katika kazi yako uifanyayo… !! Amen.
Naam, huyo ndiye
Miss Yunar ambaye leo nimefanya naye Interview ili kuweza kujua yeye ni nani na
anafanya nini.. Tumpe support basi ili aweze kufika pale ambapo anahitaji
kufika katika tasnia hii ya muziki hapa nchini na kimataifa pia. Miss Yunar
ameongea mengi sana ila kikubwa anasema
kuwa bila wewe hakuna Yunar.
Usikilize kwa umakini wimbo huu NISAMEHE by Miss Yunar ft Ben Pol na utagundua kipaji halisi cha mwanadada Miss Yunar Magicion.
No comments:
Post a Comment