UNIC NA TAYODEA WAENDESHA SEMINA YA KUPINGA MATUMIZI NA BIASHARA YA MADAWA YA KULEVYA JIJINI TANGA
Afisa
uhusiano wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Usia Nkhoma
Ledama akiwasilisha ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu
siku ya kimataifa ya kupinga matumizi na biashara haramu ya madawa ya
kulevya kwenye kongamano la vijana kuhusu madawa ya kulevya mjini Tanga.
Afisa habari wa kituo cha taarifa cha Umoja wa mataifa (UNIC) Usia
Nkhoma Ledama akikabidhi Beji ya utambulisho kwa mmoja wa vijana
aliyekaa miezi sita kwenye nyumba ya mafunzo ya waathirika wa madawa ya
kulevya bila kutumia madawa hayo mjini Tanga katika kituo cha Tanga
Sober House.
Pichani
juu na chini ni baadhi ya vijana wakifuatilia semina ya kupinga
matumizi na biashara haramu ya madawa ya kulevya iliyoandaliwa na Kituo
cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) kwa kushirikiana na TAYODEA.
Ujumbe
kutoka Ofisi za Umoja wa Mataifa Dar es Salaam, waandishi wa habari na
watumiaji wa dawa za kulevya walioonyesha nia ya kuacha kutumia dawa
hizo mjini Tanga, ambao wapo kwenye nyumba ya mafunzo ya kuwawezesha
kuachana na dawa hizo (TANGA SOBER HOUSE) iliyopo Tanga. Ikiwa ni sehemu
ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupinga matumizi na biashara ya
dawa za kulevya ambayo hufanyika 26 June kila mwaka. Kitaifa maadhimisho
hayo yanafanyika mjini Dodoma.
No comments:
Post a Comment