WANAFUNZI WALIOSOMA SHULE ZA KATA VYUO VIKUU WAMTAKA LOWASSA AWANIE URAIS 2015
Mbunge
wa Monduli, ambaye pia ni waziri mkuu mstaafu, Edward Lowasa,
akisalimiana na wanafunzi wa chuo kikuu cha UDOM waliotoka shule za
sekondari za kata, wakati walipofika nyumbani kwake mkoani Dodoma kutoa
shukrani zao kwa hatua waliyofikia kielimu.
Hamida Salum mwanafunzi wa mwaka wa kwanza UDOM, akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mh.
Lowasa katikati, Dkt. Mahanga (Kulia) na Parseko Korne wakiwa katika
picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi hao.
WASANII WATAMBA TAMASHA LA FILAMU LA GRAND MALT
Na Mwandishi Wetu
WASANII
mbalimbali watakaoshiriki katika Tamasha la Tamasha la Wazi la Filamu
Tanzania, maarufu kama ‘Grand Malt Tanzania Open Film Festival’ ambalo
litafanyika katika Viwanja vya Nyamagana jijini Mwanza, wameanza kutoa
tambo zao.
Tamasha
hilo linatarajiwa kuanza Jumatatu ijayo, ambapo kutakuwa na maonyesho
mbalimbali ya filamu pamoja na burudani za muziki kutoka bendi ya Extra
Bongo, pamoja na ngoma za asili.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti, wasanii hao walisema tamasha hilo litawafungua
macho wengi ikiwa pamoja na kupata kujua kile ambacho wanakifanya wakati
wakirekodi sinema zao.
Msanii
mahiri wa filamu, Aunty Ezekiel alisema atakuwepo Mwanza kipindi chote
cha tamasha hilo na akataka mashabiki wafike kwa wingi kushuhudia filamu
kali zaidi ambazo amezicheza katika siku za karibuni, ambazo
zitaonyeshwa bure.
“Mimi
ndiye mkali wao, Watanzania waje kushuhudia kile ambacho tumekifanya,”
alisema Aunty Ezekiel, kauli ambayo iliungwa mkono na Jacqueline Wolper
aliyedai naye atakuwepo, ila ndiye pia anayejiamini ni ‘mzuri’ zaidi
katika mambo ya filamu.
Irene
Uwoya alitamba atafunika wengi katika tamasha hilo, huku Vicent Kigosi
‘ray’ na Jacob Steven ‘JB’ nao wakijinasibu watafanya vitu adimu zaidi
katika tamasha hilo linalosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wengi wa
filamu hapa nchini.
Mkurugenzi
wa Extra Bongo, Ally Choki alitamba watafanya kweli zaidi siku ya
uzinduzi kwani watapiga vibao vipya na kutoa shoo mpya kwa mashabiki
watakaojitokeza kipindi chote cha tamasha hilo.
“Tumejiandaa
vya kutosha, tuna shoo mpya na ya aina yake, ambayo si ya kukosa. Waje
tu waone Extra Bongo itakachofanya ni nini,” alisema Choki.
Mratibu
wa Tamasha hilo aliye pia Mkurugenzi wa Sophia Records, Musa Kissoky,
alisema kwa sasa kinachosubiriwa ni siku ya tamasha tu na kusema wasanii
wengi wa filamu watakuwepo hapo.
“Kwa
sasa maandalizi yamekamilika kwa asilimia 90, yaani tunaleta kitu
tofauti ambacho watu watashangaa, ndio maana mpaka sasa wengi wanapigwa
na bumbuwazi kuhusu kile tutakachofanya siku hiyo,” alisema.
Naye
Meneja wa kinywaji cha Grand Malt walio wadhamini wakuu wa tamasha
hilo, Consolata Adam, alisema wameamua kufanya kweli zaidi kwani
wanataka kuona Watanzania wanapata kitu chenye uhakika.
“Tumejipanga
katika hili na wala hatutanii kwani tunataka kuwawezesha wakazi wa
Mwanza na maeneo ya jirani kuhudhuria tamasha hili kwa wingi .
Tunawakaribisha watu wote wenye mapenzi na filamu zetu za Tanzania
kufika na kushuhudia tamasha hili ambalo mwaka huu limeboreshwa zaidi,”
alisema Consolata.
Tamasha
la Filamu la Grand Malt linatarajiwa kuanza Julai 1-7, mwaka huu huku
kukiwa na filamu mbalimbali zitakazooneshwa katika kipindi hicho. Filamu
zote hizo ni kutoka Tanzania.
Tamasha
hilo la filamu limedhaminiwa na kinywaji cha Grand Malt kisicho na
kilevi ambacho kinazalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania
(TBL) kwa kushirikiana vyema na ISAMILO LODGE ya Mwanza.
No comments:
Post a Comment