MAADHIMISHO YA SIKU YA UGONJWA WA SIKOSELI DUNIANI, YAFANYIKA JIJINI DAR
Mwenyekiti
wa Mfuko wa Sikoseli Tanzania, Grace Rubambey (katikati) akizungumza
wakati wa maadhimisho ya Siku ya ugonjwa wa Sikoseli Duniani jijini Dar
es Salaam. Wengine kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Mfuko
huo, Dk Julie Makani, Balozi wa Canada nchini, Alexandre Leveque na
mmoja wa watu wanoishi na ugonjwa huo, Arafa Salim Said.
Balozi
wa Canada nchini, Alexandre Leveque (katikati) akizungumza wakati wa
maadhimisho ya Siku ya ugonjwa wa Sikoseli Duniani jijini Dar es Salaam
leo. Wengine kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Mfuko wa Sikoseli
Tanzania Dk Julie Makani na Mwenyekiti wa mfuko huo, Grace Rubambey na
mmoja wa watu wanoishi na ugonjwa huo, Arafa Salim Said.
Makamu
Mwenyekiti wa Mfuko wa Sikoseli Tanzania, Dk Julie Makani (kushoto)
akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya ugonjwa wa Sikoseli Duniani
jijini Dar es Salaam. Tanzania ni nchi ya nne duniani kwa kuwa na
idadi kubwa ya watu wanaougua ugonjwa wa sikoseli.
Meneja
wa Benki ya KCB Tawi la Msimbazi, Philipo Pilla (kulia) akizungumza
wakati wa maadhjimisho hayo. Benki ya KCB ni mmoja wa wadhamini wa Mfuko
wa Sikoseli Tanzania.
Mratibu wa Huduma za Ugonjwa wa sikoseli katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Dk. Deogratias Soka (kulia)
akizungumza kuhusu hali ya ugonjwa huo katika hospitali hiyo katika
maadhimisho hayo. Inakadiriwa kuwa katika ya watoto 8,000 hadi 10,000
kuzaliwa na ugonjwa huo nchini Tanzania kila mwaka.
Baadhi
wa watu walioshiriki maadhimisho jijini Dar es Salaam leo. Ugonjwa wa
sikoseli ni ugonjwa wa kurithi unaosababisha mabadiliko yasiyo ya
kawaida katika chembechembe nyekundu za damu hivyo mtu hawezi
kuambukizwa kwa njia yoyote ile kama vile kuishi au kuwa karibu na
mgonjwa wa sikoseli.
No comments:
Post a Comment