Nani anayefanya Uharamia huu?
Lakini
nani anayefanya Uharamia huu? Nani anauruhusu ufanyike? Hata kama
Serikali imeshindwa, Hivi Mungu naye anaweza kushindwa kumshughulikia
huyu anayemwaga damu za watu zisizo na hatia? Hashindwi!.
Najiuliza
kila yanapotokea matukio kama mawili ya Arusha, ambapo Mabomu yalitupwa
na mtu makusudi, kiasi cha kuua na kujeruhi watu waliofanywa kuwa Vilema bila kutarajia!
Anayefanya hayo ana Wazazi, ndugu na Jamaa zake? Je mtu huyu ana Mke au
Mume na Watoto? Huyu mtu kweli ana Wakwe zake? Ana uhai na anapumua
kama wandamu? Maana huyu si wa kawaida! Labda ni Shetani anayekunywa
damu za watu!
Namshangaa
mtu huyu asiyeona huruma damu zikimwagika, viungo vya watu
vikisambaratika ardhini na damu zao zikidonolewa na ndege, Kuku na
wadudu, huku yeye akifurahi moyoni mwake!
Labda
mtu huyu hana makazi mbinguni (Ahera), ameshakataliwa na Mungu, hivyo
anazungukazunguka kama simba aungurumaye ili kutafuta Mtu ammeze! Na kwa
hasira ya kukataliwa, ndiyo maana anaamua kufanya uharamia akidhani
atawapata wa kwenda nae. Amekosa!
Marehemu
Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kusema, “Mtu akisha kuonja
kula Nyama ya Mtu, akaona ni tamu, hataacha, ataendelea kula tu hata
akivimbiwa hatatosheka” inaonekana Uharamia wa kutafuna Nyama za watu,
hajatosheka!
Vyombo
vya Dola, Wenyeviti wa Ulinzi na Usalama wa Wilaya, Mikoa na Taifa,
inaonesha wameshindwa kudhibiti uharamia huu unajitokeza kila siku
inapoitwa leo. Ushahidi wa kushindwa, ni vitendo hivyo kujitokeza pamoja
na kuwepo walinzi.
Tujiulize!
Je bado Vyama na Wananchi, wawe na Imani navyo na kuomba ulinzi kwao?
Kama watu wanafanya uharifu wa uharamia wa kigaidi mbele ya vyombo
hivyo? Kama uharamia umefanywa machoni mwao, alaumiwe nani?
Tusemeje!
Kama Uharifu na Uharamia wa namna hii unaendelea kufanywa Machoni mwa
Serikali ya Chama cha Mapinduzi na Vyombo vyake vya Usalama na kumnusuru
Mharifu, wananchi tuwe na Imani Ipi?
Awali
Bomu lililolipuka katika mkusanyiko wa watu, Mei 5 mwaka huu katika
Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasit mjini
Arusha na kuua watu watatu na wengine kujeruhiwa, tulisema ni bahati
mbaya. Je hili ambalo ulinzi umeombwa!
Nia
Nzuri ya Serikali ya CCM kutaka mikutano ya hadhara inapofanyika
taarifa zitolewe kwa vyombo vya Usalama, ni kusudi likitokea Jambo,
vyombo vya usalama viwe na sababu ya kuulizwa na kuwajibika kukabiliana
nalo!
Sasa
vibali viliombwa na ruhusa ikatolewa, uharamia umetokea mikononi mwa
ulinzi wa vyombo hivyo! Je ashikiwe bango nani? Basi kikosi kizima
kilichohusika na ulinzi kwenye mkutano huo viwajibike pamoja na mkuu
wao! Maana vimeshindwa kulinda.
Aidha
kabla hatujailaumu Serikali na CCM, CCM iiwajibishe Serikali na
Serikali iliwajibisha Polisi na Vyombo vyake, maana vimeshindwa
kutekeleza wajibu wake na kusababisha maisha ya watu kupotea bila ya wao
kumpoteza Mharamia! Lau mmoja wao!
Ni
rai yangu kwa wananchi, Ninyi ndio Walinzi wazuri wa Amani ya Tanzania,
hivyo nawashauri wasidanganyike na Kamga na Kofia na lolote, iwapo
wataamua Kuta za Yeriko zianguke, basi wanaweza 2015 wakazunguka Yeriko
mara Saba na Kulia Huleee! Kuta zitaanguka!
Nasema nikirejea! Mungu hashindwi kumpata anayesababisha vilio vya watanzania vitoe machoni mwao!
No comments:
Post a Comment