RAIS WA TFF LEODGER TENGA WATAKA MAKOCHA WALIOMALIZA KOZI KUIBUA VIPAJI VYA SOKA NCHINI
Mhitimu
wa kozi ya ukocha wa mpira wa miguu kwa ngazi ya pili, Seleman Matola
akipongezwa na Rais wa Shirikisho la Soka nchini, Leodgar Tenga kwenye
sherehe zilizofanyika Uwanja wa Taifa. Kulia ni Mwenyekiti wa DRFA
Almas Kassongo na (kushoto) Mkurungenzi wa Ufundi TFF, Sunday Kayuni.
***********************************
RAIS
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodger Tenga,
amewataka makocha kuhakikisha wanaibua vipaji vya watoto ili kuwa na
vipaji vingi baadaye.
Tenga
alikuwa mgeni rasmi katika ufungaji wa kozi hiyo ya ngazi ya pili
iliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kozi
hiyo iliyoendeshwa na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa Dar es Salaam
(DRFA), ilianza Juni 3 huku ikishirikisha zaidi ya makocha 58.
Tenga
alisema Bara la Afrika ndilo bara lenye upungufu mkubwa wa wachezaji
watoto, tofauti na mabara mengine, kitu ambacho kinarudisha nyuma
maendeleo ya soka.
“Hili
ndilo bara ambalo lipo nyuma katika kuibua vipaji, mfano nchi ya
Ujerumani pekee ina watoto zaidi ya milioni moja ambao wanaandaliwa,
lakini hapa sijui kama wanafika hata idadi hiyo, hivyo kuna changamoto
kubwa katika hilo,” alisema.
Aliwataka
kuhakikisha wanayatumia mafunzo hayo katika kuleta mabadiliko katika
soka hapa nchini, ambapo pia aliwapongeza kwa kushiriki katika kozi
hiyo.
Naye
Mwenyekiti wa DRFA, Almas Kassongo amesema kozi hiyo itakuwa mkombozi
wa makocha kusaidia timu zao kufanya vizuri na kuendeleza mchezo huo
nchini.
"Napenda
kutoa shukrani zangu za dhati kwa Rais wa TFF kwa kukubali kuwa nasi
licha ya majukumu mengi aliyonayo, lakini niseme tu kwamba kozi hii
imekuwa ya mafanikio kutokana na kushirikisha wachezaji wengi wa
zamani," alisema.
Baadhi
ya washiriki waliohitimu kozi hiyo ni pamoja na Moses Mkandawile,
Shedrack Nsajigwa, Ibrahim Masoud Maestro, Shaffih Dauda, Rahel
Pallangyo, Ally Yusuph Tigana, Emanuel Gabriel, Jemedari Said, Benard
Mwalala, Edibily Lunyamila, Seleman Matola na wengineo.
TANZANIA YASHINDA TUZO 3 ZA UTUMISHI WA UMMA BARANI AFRIKA NCHINI GHANA.
Tanzania imeshinda tuzo tatu za juu za ubunifu katika Utumishi wa Umma, barani Afrika, kufuatia Tasisi tatu za Tanzania, kushinda nafasi ya kwanza, na kukabidhiwa vikombe vya ushindi na rais wa Ghana, wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Utumishi wa Umma barani Afrika, yaliyofanyika jana mjini Accra nchini Ghana.
Taasisi za Tanzania zilizoshinda ni Ofisi ya Ukaguzi ya Taifa, (NAO), Wakala wa Vipimo, (WMA), na Wakala wa Vitambulisho vya Taifa, (NIDA) kufuatia kufanya vizuri katika maonyesho ya siku 7 ya shughuli mbalimbali za utumishi wa umma yaliyofikia kilele tarehe 23/06/2013.
Akiuzungumzia ushindi huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Mhe. Celina Kombani, amezipongeza taasisi hizo, zilizolitea sifa taifa hili na kuelezea kufarijika kwake na ushiriki wa mkubwa wa Tasisi za Tanzania katika maonyesho hayo ambapo jumla ya taasisi 42 kutoka Tanzania, zilishiri.
Akisoma hotuba katika kilele cha maandimisho hayo, Mhe. Kombani ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mawaziri wa Utumishi Barani Afrika, amewataka watumishi wa umma kote barani Afrika, kuwatumikia wananchi kwa bidii,
unyenyekevu, uadilifu wa hali ya juu, na kueleza utumishi wa umma ni kuwatumikia watu.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Gearge Yambesi, amekiri kuwa Tanzania ni moja ya nchi zinazofanya vizuri sana katika utumishi wa umma barani Afrika, hali inayofanya Tanzania kujijengea heshima kubwa barani Afrika na Ulimwenguni kwa ujumla.
Wakizungumzia kuhusu ushiriki wa Tanzania katika maonyesho hayo, Waziri , Mhe. Celina Kombani, na Katibu Mkuu, Bwana. George Yambesi, wanaeleza zaidi.
Akizungumzia maonyesho hayo, Mkurugenzi wa Kampuni ya Press and Public Relations (PPR), Bw. Pascal Mayualla, amesema mfulululizo wa vipindi vya redio na Televisheni, kuhusu ushiriki wa Tanzania, katika Maonyesho ya Utumishi wa Umma barani Afrika, vitaanza kuonekane kesho, katika vituo mbalimbali vya redio na Televisheni.
WANAWAKE WANA UWEZO WA KUBADILISHA MAISHA YA MTANZANIA
Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa Kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya wanawake wajasiriamali yanayoendelea kwenye ukumbi wa Bwalo la Maafisa la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT),Mgulani jijini Dar es salaam.
***************************************
WANAWAKE
wakiwezeshwa kiuchumi na kupatiwa elimu ya msingi ya ujasiriamali,
kuepuka maradhi hatarishi na kufahamu haki zao katika jamii, umasikini
utapungua, kipato kitaongezeka na maisha ya Watanzania yatabadilika.
Hayo yalisemwa
leo na Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa Kwa Wote (EOTF), Mama Anna
Mkapa wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya wanawake
wajasiriamali yanayoendelea kwenye ukumbi wa Bwalo la Maafisa la Jeshi
la Kujenga Taifa (JKT),Mgulani jijini Dar es salaam.
Mama
Anna Mkapa ambaye pia ni Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin
Mkapa alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wa kiuchumi
na kijamii wajasiriamali hao kutoka mikoa yote Tanzania Bara na
Visiwani, ambapo jumla ya wanawake wapatao 264 wanashiriki.
“Mfuko
wa Fursa Sawa Kwa Wote umekusudia kwa nguvu zake zote kuendeleza vita
ya hii ya kuwawezesha wanawake nchini kujikwamua katika wimbi la
umasikini, maradhi na ujinga,” alisisitiza Mama Mkapa.
Aidha
ameiomba Serikali, Asasi za kiraia, taasisi za dini, wahisani binfasi
ndani na nje ya nchi, kusaidia wanawke haswa wa vijijini kujikwamua
na umasikini.
Mama
Mkapa aliongeza kuwa mfuko huo, kwa kipindi cha miaka 16 zaidi ya
wanawake 6,820 wamepata mafunzo ya stadi za biashara na wengine 4,500
wamepata fursa ya kushiriki maonyesho mbalimbali ya ndani na nje ya nchi
kwa kupitia EOTF ili kutangaza na kuuza bidhaa zao.
Naye
Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko Dk. Abdallah Kigoda akifungua
mafunzo hayo alisema Serikali imeanzisha utaratibu wa kuweka kumbukumbu
za mkopo katika mabenki kwa kupitia ‘Credit Reference Bureau’ ili
kuweza kusaidia kuwafahamu wateja, na kuwaasa wajasiriamali wanapokopa
wakumbuke kulipa kwani uaminifu ni kitu muhimu katika biashara.
“Suala
lingine la kulipa kipaumbele ni lile la kuongeza thamani ya mazao
wanayoyazalisha na tuache kuwazalishia watu wengine bidhaa
wakaenda kuongezea thamani kidogo tu kama vile kwa kufunga na kuweka
nembo ya kibiashara na kuuza kwa bei kubwa,” alisema Dk. Kigoda.
Aliahidi kuwa Wizara yake iko makini kufanya linalowezekana kushirikiana na wajasiliamali hao kutatua tatizo hilo la kuuza malighafi badala ya bidhaa iliyoongezwa thamani ili kuongeza ajira na kupunguza umasikini.
No comments:
Post a Comment