MCHEZAJI WA CROATIA ALEN PAMIC AFIA UWANJANI
Wachezaji
wa timu ya Crotia, wakimsaidia mchezaji mwenzao, Alen Pamic
(aliyelala), wakimpatia huduma ya kwanza na katika moja ya mechi
alizowahi kuzimia uwanjani hivi karibuni kutokana na matatizo ya ugonjwa
wa moyo.
****************************************
Hivi
karibuni, Pamic alipoteza fahamu katika mechi ya ligi dhidi ya
Lokomotiva iliyopigwa Februari, ambapo licha ya matatizo yake hayo
alisisitiza kuendelea kucheza soka, huku madaktari wake wakimruhusu
kufanya hivyo
NYOTA
wa soka la kulipwa raia wa Croatia, Alen Pamic ameanguka uwanjani na
kufariki dunia wakati wa mechi ndogo isiyo ya kimashindano, gazeti la
kila siku la Vecernji List limesema katika toleo lake mtandaoni la leo
Jumamosi.
Taarifa
hiyo imeripotiwa kwa ufupi, huku ikiwa haina maelezo zaidi kuhusiana na
kifo cha Pamic aliyekufa akiwa na umri wa miaka 23 tu.
Pamic,
aliyekuwa akichezea klabu ya NK Istra 1961 katika ligi ya daraja la juu
zaidi nchini hapa, alikuwa na historia ya matatizo ya moyo, ambayo
yalimwangusha dimbani mara tatu kabla ya tukio hilo lililochukua uhai
wake.
Hivi
karibuni, Pamic alipoteza fahamu katika mechi ya ligi dhidi ya
Lokomotiva iliyopigwa Februari, ambapo licha ya matatizo yake hayo
alisisitiza kuendelea kucheza soka, huku madaktari wake wakimruhusu
kufanya hivyo.
Pamic
aliyekuwa kiungo mahiri dimbani, aliutumia msimu mmoja wa 2010/11
kuchezea klabu ya Standard Liege ya Ligi Kuu ya Ubelgiji, lakini klabu
hiyo ikamtema muda mfupi baada ya kupata shambulio la moyo na kuzimia
akiwa mazoezini, gazeti la Vecernji limesema katika taarifa yake.
Pamic
ni mtoto wa nyota wa zamani wa kimataifa wa Croatia, Igor Pamic, ambaye
kwa sasa anainoa klabu ya NK Istra 1961 aliyokuwa akiichezea marehemu.
Souse:- Supersport.com
No comments:
Post a Comment