Thursday, June 13, 2013

Haya ni maoni ya Jaji Bomani kuhusu ishu ya Serikali tatu

.
.
Najua bado ishu ya rasimu ya katiba mpya iko kwenye headlines Tanzania ambapo time hii Mwanasheria mkuu mstaafu wa Serikali Jaji Mack Bomani nae ametoa msimamo wake kuhusiana na muundo wa serikali na kuamplfy kwamba ni vizuri katiba mpya iutambue muundo wa serikali tatu kama ilivyopendekezwa na tume ya kuratibu maoni inayoongozwa na Jaji Joseph Warioba.

Jaji Bomani anasema alipata fursa ya kutoa maoni yake na kupendekeza muundo huo ambao utasaidia kutatua baadhi ya kero za muungano ikiwemo mgawanyo wa mapato ambao kwa muda mrefu umekua ukilalamikiwa.

Namkariri akisema “Wananchi wanatakiwa waachiwe waamue wenyewe muundo gani wa Serikali wanautaka kwa kupiga kura badala ya kuwaamulia, tuunde sasa Muungano au shirikisho la serikali tatu… moja Zanzibar, Tanganyika na nyingine ya Muungano, wametoa sababu zao nyingi na nzuri zipo kwenye hii rasimu, mimi nilifikisha maoni yangu mbele ya tume hiyo kwa jambo ambalo nalielewa fika”
Jaji Bomani ametoa haya maoni siku moja baada ya CCM kusema itatangaza msimamo wake baada ya kukusanya maoni ya Wanachama wake na uamuzi utakaofikiwa.
.
.

No comments:

Post a Comment