Friday, March 29, 2013


*TIMU YA IKULU DAR ES SALAAM NA TIMU YA IKULU ZNZ ZATAKIWA KUDUMISHA USHIRIKIANO

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Dk.Mwinyihaji Makame Mwadini,akizungumza na wanamichezo wa Ikulu ya Dar es Salaam na wa Ikulu Zanzibar,kwa niaba ya Rais wa Zanzibar,ikiwa ni sehemu ya kudumisha ushirikiano zaidi kupitia michezo mbali mbali itakayochezwa katika kipindi cha wiki ya Pasaka. Michuano hiyo inafanyika mjini Zanzibar.
 Makamo Mwenyekiti wa Timu ya michezo ya Ikulu ya Dar es Salaam George Mwakilana,alipokuwa akitoa salamu za Ikulu ya Dar kwa uongozi wa Tmu ya Ikulu ya Zanzibar,wakati wa Mkutano wa  Timu hizo,wakati mazungumzo ya kutakiana kheri katika michezo mbali mbali itakayochezwa katika kipindi hichi cha wiki ya Pasaka inayofanyika Zanzibar.
Wanamichezo wa Ikulu ya Zanzibar na Dar es Salaam wakisikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Mwinyihaji  Makame Mwadini, akizungumza nao katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifan SUZA jana
 Timu za Michezo za Ikulu ya Zanzibar wenyeji na Ikulu ya Dar es Salaam,zikiwa katika picha ya pamoja baada ya mazungumzo ya kuwakaribisha Timu ya Ikulu Dar,ambapo  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Mwinyihaji  Makame Mwadini,aliwakaribisha kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein. Picha na Ramadhan Othman,Ikulu

No comments:

Post a Comment