Sunday, March 31, 2013

KUMEKUCHA MISS TABATA 2013

 
Uzinduzi wa shindano la kumtafuta Miss Tabata 2013 unafanyika leo Da West Park, Tabata jijini Dar es Salaam.

Katika uzinduzi huo, jumla ya walimbwende 26 watambulishwa kwa mashabiki kwenye onyesho hilo ambalo litaenda sambamba na kusherekea sikukuu ya Pasaka.

Mratibu wa shindano hilo, Joseph Kapinga alisema jana kuwa warembo hao watatambulishwa pamoja na washiriki wa Miss Mzizima.

Kapinga aliwataja warembo wa Tabata watakaotambulishwa kuwa ni Martha Gewe (19), Zilpha Christopher (19), Hidaya David (22), Aneth Ndumbalo (19), Amina Ally (18), Dorice Mollel (22), Eunice Nkoha (19), Kazunde Kitereja (19), Angela Fradius (19), Domina Soka (21), Rehema Kihinja (20), Glory Jigge (18) na Sophia Claud (21).

Aliwataja wengine ni Lilian Mpakani (19), Lilian Msanchu (19), Rita Frank (20), Pasilida Mandali (21), Rachel Mussa (19), Jasmin Damian (18), Angelina Mkinga (19), Mercy Mwakasungu (20), Tunu Hamis (19), Blath Chambia (23), Ray Issa (22), Shamim Abass (22) na Shan Abass (22).

No comments:

Post a Comment