Friday, March 29, 2013

RAIS JAKAYA KIKWETE, MAKAMU WAKE DKT. BILAL, WAZIRI MKUU, MIZENGO PINDA WASHIRIKI KUAGA MWILI WA ALIYEKUWA MBUNGE WA CUF DAR

 Rais Jakaya Kikwete, akiweka saini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chambani CUF, Salim Hemed Khamis, aliyefariki dunia jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa baada ya kuuguaa ghafla wakati akiwa katika Kikao cha Kamati ya Bunge cha Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika Ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam juzi. Marehemu mefariki kwa ugonjwa wa shinikizo la damu.
 Katibu wa Bunge la Jamhuri, John Joel, akisalimiana na Samuel Sitta, katika Ukumbi wa Karimjee wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu Salim Hemed Khamis, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chambani Visiwani Pemba kupitia CUF, aliyefariki jana mchana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Shughuli za kuaga mwili wa marehemu zimefanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
 Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri Mstaafu, Edward Lowasa, na viongozi wengine wakishiriki shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Salim Hemed Khamis, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chambani Visiwani Pemba kupitia CUF, aliyefariki jana mchana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Shughuli za kuaga mwili wa marehemu zimefanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya ndugu wa marehemu wakati viongozi wakiondoka kwenye ukumbi wa Karimjee baada ya kushiriki katika shughuli za kuaga mwili wa marehemu, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chambani Visiwani Pemba, Salim Hemed Khamis (CUF), aliyefariki jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
 Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) William Lukuvi, na Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Adam Malima, wakizungumza nje ya ukumbi wa Karimjee, baada ya kushiriki shughuli ya kuaga mwili wa marehemu,Salim Hemed Khamis, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chambani Visiwani Pemba kupitia Chama cha CUF, aliyefariki jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Waombolezaji wakibeba jeneza lenye mwili wa marehemu,Salim Hemed Khamis, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chambani Visiwani Pemba kupitia Chama cha CUF, aliyefariki jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, wakiingiza kwenye gari tayari kuelekea uwanja wa ndege kwa safari ya kuelekea Pemba kwa maziko.

No comments:

Post a Comment