Sunday, March 31, 2013

MIILI YA WATU 24 YAPATIKANA KWENYE GHOROFA LILILOANGUKA DAR MPAKA SASA,UOKOAJI BADO UNAENDELEA.

Miili ya watu iliyoopolewa kutoka kwenye vifusi vya jengo lenye ghorofa 16 lililoanguka jana katikati ya jiji la Dar es Salaam, imefikia 24.

Shughuli za uokoaji zilizoanza jana bado zinaendelea kwa siku ya pili huku kukiwa na taarifa za kuwepo miili zaidi kwenye vifusi hivyo.

Jana Rais Jakaya Mrisho Kikwete alitembelea katika eneo la jengo hilo lililoporomoka lililopo Mtaaa wa Indira Gandhi/Morogoro.

No comments:

Post a Comment