Sunday, March 24, 2013

MOJA KATI YA STORI MUHIMU ZA KIJAMII WIKI HII

.
Balozi wa Canada ndio alikua mgeni rasmi.

Taarifa ikufikie kwamba Shirika la Under The Same Sun kuanzia April 2013 itatangaza mfululizo wa vipindi vya elimu “Tambua Albinism” vitakavyokua vinasikika kupitia redio za jamii za kanda ya ziwa kwenye mtindo wa makala mchanganyiko, majadiliano ya moja kwa moja ikiwa ni pamoja na mchango wa simu kutoka kwa wanaosikiliza.

Ni mradi ambao unafadhiliwa kwa ushirikiano wa serikali ya Canada kupitia ubalozi wa Canada Tanzania na shirika la Under The Same Sun ambapo lengo ni kuongeza uelewa wa jamii kuhusu Albinism kama hali ya kurithi na changamoto zinazowakabili watu wenye Albinism, kuondoa mila potofu kuhusu Albinism, kuendesha kampeni kupunguza na kukomesha ubaguzi dhidi ya watu wa aina hii, kuhamasisha wazazi na watoa huduma jinsi ya kuwatunza na kuwalea watoto wenye Albinism pamoja na kutetea haki na ustawi wa watu hawa.

Sengerema Fm, Sibuka Fm, Faraja Fm, Fadeco Fm, Kahama Fm na Chemchemi Fm ni baadhi ya radio zitakazohusika na vipindi hivi.
.
Balozi wa Canada Tanzania ndio alikua mgeni rasmi.
.
.
.
.

No comments:

Post a Comment