Sunday, March 24, 2013

HII HABARI YA NANCY SUMARI IMEINGIA KTK HABARI 20 BORA ZA WIKI

Jacqueline Ntuyabaliwe, Nancy Sumari na Faraja Nyalandu.
Jacqueline Ntuyabaliwe, Nancy Sumari na Faraja Nyalandu.

Stori ya Miss Africa 2005 mrembo Nancy Sumari ilishika nafasi ya tatu kwenye habari kumi bora za jumanne march 29 2013 kwenye AMPLIFAYA ya CLOUDS FM ikiwa ni stori iliyozungumziwa kwa dakika 4 na sekunde kumi hewani, hiyo yote ni kutokana na uzito wa habari yenyewe ambapo pia baada ya tathmini, imeshika nafasi ya 6 kati ya habari 20 za wiki iliyokwisha.

Kama ilikupita, ni kwamba Nancy Sumari alizindua kitabu chake cha kwanza march 19 2013 Dar es salaam kinachoitwa ‘Nyota Yako’ ambacho kimelenga kuwazungumzia Wanawake wakubwa na wadogo tofautitofauti kwenye jamii na nafasi zao akiwemo Shujaa Bibi Titi Mohameda jinsi wanavyojitahidi kuleta mabadiliko na kuwahamasisha wanawake wengine kuona kwamba maendeleo yanawezekana.
.
Mgeni rasmi alikua huyu Daktari wa kwanza mwanamke Tanzania.

Namkariri Nancy Sumari akisema “mtoto ambae yuko shule ya msingi anaweza akamwangalia Bibi Titi na kufananisha historia yake na akajifananisha kwa maana ya kujiamini kutaka kufanya zaidi kwenye maisha yake na kuweza kupigania haki zake na Wanawake wengine”

Kwenye Exclusive interview aliyofanya na millardayo.com Nancy alijibu swali aliloulizwa kama amehusisha historia yake ndani ya kitabu hiki ambapo alijibu “hapana sijaandika historia yangu kwa sababu natarajia kuandika kitabu kingine tena, yani huu ni mwanzo wa vitabu vingine vitakavyokuja kwa hiyo kwa kuanzia nilitaka kutoa nafasi kwa Wanawake wengine ambao kuna uwezekano tusingewasikia, nimeanza kukiandika toka mwaka jana”
.
Jacqueline Ntuyabaliwe na Fashion designer Ally Remtullah walikua sehemu ya waliokuja kutoa support kwa Nancy.

Hiki kitabu kitapatikana kwenye maduka mbalimbali ya vitabu Tanzania ambapo kingine kizuri alichonifurahisha Nancy ni kwamba atakigawa bure kwenye maktaba mbalimbali za shule tofauti za msingi Tanzania ili watoto wa kike wapate nafasi ya kukisoma, sasa hivi kuna michango ya marafiki tayari imeshatolewa ili kazi ya kuendelea kukichapisha iendelee”
.
.

No comments:

Post a Comment