Saturday, March 30, 2013

.
Hii ndio page sahihi ya facebook.

Taarifa ikufikie kwamba kuna watu wanatumia vibaya jina la mwanamitindo wa kimataifa Flaviana Matata katika mtandao wa kijamii wa Facebook kwa kuwarubuni wasichana, kuna ukurasa feki unaitwa Flaviana Matata’s,

Watu hawa huwarubuni wasichana na kuwaahidi kuwatafutia kazi nje ya nchi kwa mgongo wa Mwanamitindo huyu, wanasema kuna kaka yake Flaviana ambaye hukutana na wasichana hawa na baada ya mazungumzo anawalaghai kwa njia mbalimbali., pia wahusika hawa hutoza kiasi cha pesa hata kufikia shilingi laki mbili (200,000 ) kama tozo kwa huduma hii ya kuwatafutia kazi nje ya nchi.

Compass Communications kama kampuni inayosimamia kazi za Flaviana Matata inatoa tahadhari kwamba Flaviana hausiki kwa njia yoyote na hiyo page wala hafahamiani na watu hao, pia watu wawe makini kwa sababu Flaviana Matata hayuko katika biashara ya kumtafutia mtu yoyote kazi ya Uwanamitindo popote, ukurasa halisi wa Flaviana Matata kwenye Facebook ni huo hapo juu wa “Flaviana Lavvy Matata”
Jitihada za kuendelea kufatilia wanaohusika ili kukamatwa zinaendelea, toa ushirikiano unapopata taarifa yoyote

.
Hii sio yake

No comments:

Post a Comment