Saturday, March 30, 2013

KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI AFARIKI DUNIA

Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Shabani Kimea (54) amefariki dunia machi 27 mwaka huu katika Hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa kwa ajili ya matibabu ya maradhi.
Taarifa iliyotolewa na kuthibitishwa na  Msemaji wa Polisi Advera Senso, imesema Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Familia ya Marehemu tayari imefanikisha kuusafirisha mwili wa marehemu kwenda Kijijini kwao Mwera mkoani Tanga, kwa ajili ya Mazishi.

No comments:

Post a Comment