Meneja Chapa wa Tigo
Tanzania Bw. William Mpinga akiongea na waandishi wa habari kuhusu tamasha
kubwa la Tigo Mini Kabaang litakalofanyika siku ya jumapili hii bure kabisa
katika viwanja vya CCM Kirumba jijini Mwanza, kushoto msanii Diamond
Platnumz na kulia msanii Madee ambao watatoa shoo siku hiyo na wasanii wengine.
Msanii wa bongo flava Diamond
Platnumz akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu tamasha
kubwa la Tigo Mini Kabaang litalofanyika mjini Mwanza siku ya jumapili pembeni
yake Meneja Chapa wa Tigo Tanzania Bw. William Mpinga.
Msanii Madee akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu tamasha kubwa la Tigo Mini Kabaang
litalofanyika mjini Mwanza siku ya jumapili pembeni yake ni Meneja Chapa wa
Tigo Tanzania Bw. William Mpinga na Diamond Platnumz .
Msanii Richie Mavoko akizungumza
na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu tamasha kubwa la Tigo Mini Kabaang litalofanyika mjini Mwanza siku
ya jumapili kulia kwake ni Msanii Madee, meneja wa Tigo Bw. William
Mpinga na Diamond Platnumz.
Wasanii Diamond Platinumz, Madee wa Tip Top na Richie Mavoko katika picha ya
pamoja na Meneja Chapa wa Tigo Bw. William Mpinga. Wasanii wengine watakaokuwepo ni
Fid Q, Ney wa Mitego, Roma Mkatoliki,
Recho na Kazi Kwanza.
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Tamasha
la Tigo Mini Kabaang kufanyika jijini Mwanza
Dar
es Salaam, Juni 26, 2013 – Msanii Bora wa mwaka Diamond
Platnumz, Fid Q na wasanii wengine sita wanatarijiwa kupagawisha mashabiki
zaidi ya elfu sitini katika tamasha la Tigo Mini Kabaang litakayofanyika jijini
Mwanza (Rock city) Jumapili hii ya Juni 30.
Akizungumza na
waandishi wa habari kuhusu tamasha hilo, Meneja wa Chapa wa Tigo Bw. William
Mpinga alisema kwamba lengo la tamasha hilo ni kujenga mahusiano ya karibu na
wateja wao kwa kutumia sanaa ya muziki kama
njia ya kutangaza huduma za Tigo na bidhaa zake za vifurushi kwa wateja wengi
zaidi.
“Tunaamini kwamba tamasha
hili litajenga mazingira mazuri yakufanya kampuni na wateja wetu kuelewana
zaidi. Mwisho wa siku tunatarajia wateja
wetu kujumuika nasi, kupata burudani yakutosha na kuelimishwa zaidi kuhusu
huduma zetu mbali mbali zenye ubora na unafuu kama Mini Kabaang,” alisema
Mpinga.
Mini Kabaang inatoa muda
wa maongezi wa dakika 20 za bure, 50MB ya kifurushi cha intaneti, pamoja na
ujumbe mfupi 100 kwa shilingi 475 tu kwa siku.
Mkutano huo wa
waandishi wa habari pia ulihudhuriwa na wasanii wakubwa kama Madee wa Tip Top,
Ney wa Mitego, Roma Mkatoliki, Richi Mavoko, Recho, Kazi Kwanza, Diamond Platnumz
na Fid Q, ambao ndio wasanii wa Bongo Fleva watakaopamba siku hiyo ya Jumamosi katika
viwanja vya CCM Kirumba kuanzia saa 4 asubuhi mpaka saa 12 jioni.
“Mimi pamoja na wasanii
wenzangu tunayo furaha kubwa kushiriki katika tamasha la Tigo Mini Kabaang
litakalofanyika jijini Mwanza, hakika watu wa Rock city ni washabiki wakubwa wa
muziki wetu, na tunatarajia kwenda kuwapa burudani ya kutosha,” alieleza Diamond
Platnumz alipoulizwa kuhusu tamasha hilo.
“Binafsi nina furaha
yakipekee kufanya tamasha langu la kwanza la wazi jijini Mwanza. Naamini hao mashabiki
elfu sitini na zaidi wataonyesha mapenzi
ya dhati kwa muziki wangu. Ninahamu sana ya kufika na kufanya tamasha hii,”
aliongeza super staa huyo.
“Tamasha hili la Tigo
Mwanza Mini Kabaang pia litawapa fursa mashabiki kujishindia zawadi mbali mbali
kama vile simu, vocha, fulana za nembo ya Tigo na nyingine nyingi. Hakutakuwa
na kiingilio siku hiyo, tunapenda kuwakaribisha kila mteja wa Tigo na mshabiki
wa bongo fleva kujumuika na kushiriki nasi,” aliongezea Mpinga.
“MINI KABAANG” ni kifurushi cha siku ambacho mteja akijiunga anapata
dakika 20 za muda wa maongezi ambazo anaweza kuzitumia kupiga simu kwenda
mtandao wowote ule, pia anapata kifurushi cha 50MB ya intaneti na kuweza kutuma
ujumbe mfupi 100 kwa mtandao wowote. Kutumia kifurushi hiki mteja anabidi apige
namba *148*01#.
Huduma hii inapatikana kwa wateja wote wa Tigo kwa gharama nafuu ya shilingi
475 tu kwa siku.
Tamasha za Mini Kabaang ni mfululizo wa maonyesho ya muziki
yanayoandaliwa na Tigo, yamekwisha fanyika Morogoro, Moshi na sasa Mwanza. Mikoa
mengine itakayofuata ni Mbeya, Dodoma na mikoa mingine.
KUHUSU
TIGO:
Tigo
ni mtandao wa kwanza wa simu za mkononi nchini Tanzania. Ilianza shughuli mwaka
1994 na inapatikana katika mikoa ishirini na sita (26)
Tanzania
bara na visiwani.
Lengo
la Tigo ni kuwa mtandao unaoongoza kwa kutoa huduma bora na za ubunifu Tanzania
kwa wateja wake wote ambazo zinaendana na mahitaji yao kuanzia huduma za sauti
za bei nafuu, vifurushi vya intaneti vyenye kasi kubwa na huduma bora za fedha
za simu za mkononi kupitia Tigo Pesa.
International
Cellular S.A (MIC) ambayo ni ya unafuu wa huduma na inapatikana kirahisi kwa zaidi ya wateja milioni 43 katika masoko
13 barani
Afrika
na Amerika ya Kusini.
"Tabasamu upo na Tigo"
Kwa
maelezo zaidi wasiliana na:
Amani Nkurlu – Meneja Mahusiano
+255 658 870 107 au +255 712 223 839