WIZARA YA MADINI MEKEMEA MATUMIZI YA BARUTI KATIKA UCHIMBAJI MADINI
Wachimbaji wadogo wadogo wa madini katika moja ya machimbo.
WIZARA ya
Nishati na Madini hususan Ofisi ya madini
kanda ya kaskazini imekemea vikali
wachimbaji wa madini ambao wamekuwa wakitumia baruti kama silaha mbadala ya
kuzitumia kama nyenzo za kazi ya
uchimbaji.
Akizungumza na wandishi wa habari kamishna wa madini kanda ya kaskazini Mhandisi Benjamini Mchwampaka
amesema kuwa vitendo hivyo viovu vinatokana na wachimbaji wa wasiokuwa na
maadili ya uchimbaji madini ambao wanatumia baruti kutengeneza mabomu ya
kienyeji na kuwatupia wachimbaji wa migodi ya jirani.
Mhandishi Mchwampaka
ameongeza kuwa ofisi yake haitolifumbia macho suala hilo kwa kuwa huo sio uchimbaji
bali ni uhalifu kwa kuwa una lengo la kuwaumiza na kuwatisha kusudi wawafukuze
ili kuchukua maeneo yao ambayo yanahisiwa kuwa na uzalishaji wa madini.
Aidha ametaja
maeneo ambayo vitendo hivyo vimeshamiri
sana kwenye migodi inayopakana na moigodi ya Kampuni ya Tanzanite One kwenye
kitalu C.
Amefafanua kuwa
mgodi wowote ambao utabainika kwamba wachimbaji wake wanajihusisha na vitendo
vya kuwatupia mabomu wachimbaji wa migodi jirani,mgodi huo utafungwa mara moja
na leseni husika itafutwa na wahusika wote watachukuliwa hatua kali za
kisheria.
Pia amewataka
Mameneja na wachimbaji kuwa ni lazima
kutangaziana baruti ama moto kabla ya
ulipuaji baruti kufanyika ili kuthibiti
vitendo viovu.
No comments:
Post a Comment