Thursday, September 20, 2012

TASWIRA YA JIJI: Ally Hassan Mwinyi Road

Katika pita pita zangu nilikuwa barabara ya Ally Hassan  Mwinyi Mikocheni na kukutana na hii nguzo ya umeme ambayo imezungukwa na majani ambayo chini yake ni wauza miti. Sasa swali langu ni je nani anahusika katika usafi wa nguzo hizi? Ni wale watu wakusafisha barabara au hao wanaouza miti au wafanyakazi wanaoweka hizi nguzo. 

Upande mwingine huwa najiuliza maswali hawa wanaouza hii miti sehemu kama hizi za barabarani je wanatakiwa kuuza miti hiyo kwa muda gani kwa maana kuna sehemu nyingine naona ni kama pori la miti tu na wauzaji hawapo so hiyo sehemu imekuwa kama kijimsitu. Mimi nadhani ingewekwa sehemu maalumu ya kuuzia hii miti na sio kukaa barabarani na hatimaye biashara ikidoda wanakimbia na kupaacha ile sehemu inakuwa mbaya na barabara kutoleta mvuto wake.

No comments:

Post a Comment