Friday, September 21, 2012

REDD'S MISS TEMEKE 2012 KUSAKWA LEO PTA

 Warembo wanaotarajia kuchuana kwenye Ukumbi wa PTA uliopo viwanja vya Sabasaba, kuwania taji la Redd's Miss Temeke 2012.
                    
MSHINDI wa taji la Redd’s Miss Temeke 2012 katika shindano litakalofanyika katika ukumbi wa PTA, SabaSaba jijini Dar es Salaam, atazawadiwa fedha taslimu shilingi milioni 1 na vitu mbalimbali vyenye thamani ya sh 500,000.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa BMP inayoratibu shindano hilo, Benny Kisaka, alisema mshindi wa pili atapata shilingi 800,000 huku mshindi wa tatu akipata shilingi 700,000 pamoja na vitu vyenye thamani ya shilingi 500,000 kila mmoja.

Mbali ya zawadi hizo, duka la kisasa la Mariedo Boutique litatoa gauni lenye thamani ya shilingi 350,000 na kiatu cha shilingi 150,000 kwa kila mmoja kwa washindi hao watatu wa kwanza huku mshindi wa nne akipata kitita cha shilingi 400,000.

Alisema  mshindi wa tano ataondoka na kitita cha shilingi 300,000 na warembo wengine wote watakaosalia kila mmoja atapata shilingi 200,000. Taji la Redd’s Miss Temeke, kwasasa linashikiliwa na mrembo Husna Twalib.

Warembo 15 watakaochuana katika kipute hicho ni kutoka katika vitongoji vya Kigamboni, Kurasini na Chang'ombe ambapo kila sehemu wametoka warembo watano.

“Temeke imewahi kutwaa taji la Miss Tanzania mara tatu, kupitia warembo Happiness Magesse (2000), Sylvia Baham (2003) na Genevieve Mpangala, hivyo tuna uhakika warembo hawa wataiwakilisha Temeke vizuri,” alisema Kisaka.

Mbali ya kinywaji cha Redd's, Miss Temeke 2012 imedhaminiwa na City Sports Lounge, Jambo Leo, Mariedo Boutique, Global Publishers, Dodoma Wine, Push Mobile,  Mariedo Boutique, 100.5 Times FM, Kitwe General Traders, Fredito Entertainment, katejoshy.blogsport.com na 88.4 Cloud's FM.

No comments:

Post a Comment