Tuesday, September 4, 2012

MZUNGU AUNDA KUNDI LA SANAA NCHINI

    
Ronja katikati akiwa na watoto yatima mazoezini.
    
Akiwashauri mambo ya muziki wa kizazi kipya.
   
Ronja akiwa na baadhi ya wanakikundi ambao pia ni watoto yatima.…
    
Ronja katikati akiwa na watoto yatima mazoezini.
    
Akiwashauri mambo ya muziki wa kizazi kipya.
   
Ronja akiwa na baadhi ya wanakikundi ambao pia ni watoto yatima.
 
Ronja akiwa na Musa John ambaye ni mtoto yatima.
   
Baadhi ya watoto yatima wakifanya mazoezi ya muziki kwa gitaa ambalo ni mali ya studio ya mzungu Ronja.

MZUNGU mmoja raia wa Ujerumani, Krottmayer Lisa Ronja 'Lulu' amejitolea kukusanya watoto wa mtaani na kuwasaidia katika harakati za kuinua vipaji vyao vya muziki wa kizazi kipya hapa nchini. Tukio hilo limejiri hivi karibuni maeneo ya Ubungo Kibangu ambapo mzungu huyo mwenye umri wa miaka 18 amefanikiwa kukusanya vijana wengi tangu kuanzishwa kwa kundi hilo ambalo amelipa jina la “wanaharakati wa mtaa”
 
“Nimeamua kusaidia hawa vijana tunaimba nao pamoja na sasa nimewatengenezea studio ya kurekodi na tayari wameanza kuonesha harakati zao, kwa hiyo, nawapenda sana lakini natoa wito kwa wengine wajitokeze ili kupanua kundi hili, kwani sasa tuko hapa kwa ajili ya kufanya mazoezi ya kutosha, na kuinua vipaji vyao” Alisema Ronja katika moja ya harakati zake za kuwasaidia watoto wanaoishi mazingira magumu na yatima.

No comments:

Post a Comment