Saturday, December 22, 2012

*TWANGA, DIAMOND MUSICA WAKONGA VILIVYO 'TUSKER CARNIVAL' MOSHI

Bendi  za Musiki wa Dansi za Twanga Pepeta na Diamond Musica usiku wa kumkia leo ziliwapagawisha vilivyo mashabiki wa muziki huo waliofurika katika Uwanja wa Ushirika Moshi, wakati bendi hizo zilipopanda jukwaa moja na kushambulia kwa shoo kali katika Tamasha kubwa la Burudani la Tusker Carnival, jana usiku mjini Moshi.

Walikuwa ni Diamond Musica walioanza kushambulia Jukwaa hilo la Tusker Carnival, mishale ya saa mbili usilku hadi sita kasorobo walipo wapisha Wakongwe wa Burudani na Wabishi wa mjini Twanga Pepeta ambao waliwaamsha hata mashabiki waliolala.
 
Tamasha hilo la Tusker Carnival, lilianza juma lililopita jijini Dar es Salaam na baadae kupigwa jijini Mwanza huku Nguli wa Muziki wa dansi, Koffi Antonio Olomide, akiongoza mashambulizi. 

Na leo ni zamu ya jiji la Mbeya ambao watapata burudani kali kutoka kwa Mapacha wa tatu na bendi ya Watoto wa mjini Wazee wa kujinafasi A.K.A, Wazee wa Kizigo, Extra Bongo, iliyochini ya Mkurugenzi wake Ali Choki.
 Kijana wa Mjini Moshi ambaye anakula Maisha jijini Dar es Salaam akiwa na kundi la Twanga Pepeta, Mkaanga Chips, Martin 'Kibosho' Shao akiwajibika katika idara yake ndani ya Tamasha la Tusker Carnival.
 Mamaa Luwiza Mbutu akifanya makamuzi.
 Wacheza show wa Twanga Pepeta, Baby Tall (kushoto) na Zungu, wakishambulia jukwaa kwa pamoja.
 Hawa ni Diamond Musica wakishambulia jukwaa la Tusker Carnival
 Wadau wa muziki wa dansi na burudani kwa ujumla, kutoka Kampuni ya Bia ya Serengeti tawi la Mjini Moshi nao walikuwepo ndani ya Viwanja vya Ushirika Mjini Moshi na hapa wakishow LOVE ndani ya Tusker Carnival.
 Wadau wakila Bata huku wakishushia na Tusker Bardiiiiiii, ilikuwa ni burudani na makulaji katika tamasha la Tusker Carnival.
 Wadau wa Mjini Moshi nao walikuwepo uwanjanai hapo.
 Mashabiki wa bendi za Twanga na Diamond, wakisebeneka na misebene hapo kati.
 Huyu anajulikama kama Baloteli wa Bongo au Mbuyi Twitwe wa Twanga Pepeta, Mandera Sura Mbaya, akishambulia kwa staili zake za 'Kichina' katika jukwaa la Tusker Carnival mjini Moshi.
Palikuwa hapatoshi Uwanja wa Ushirika mtu nyomi zikifuatilia Burudani kutoka Tusker Carnival.

No comments:

Post a Comment