Saturday, December 29, 2012

Catherine ndiye Unique Model wa mwaka 2012

Mwanamitindo bora wa mwaka 2012 Catherine Masumbiga (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Unique Model Photogenic Elizabeth Pertty (kushoto) na Unique Model Talent Vestina Charles mara baada ya kutangazwa kwa mshindi.
Mwanamitindo wa mwaka 2012 Catherine Masumbiga (katikati) amepatikana jana usiku kwenye shindano lililofanyika kwenye Klabu ya New Maisha jijini Dar es Salaam akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa pili Cesilia Michael (kushoto) na mshindi watatu Amina Ayubu.
Washiriki waliongia tano bora.
Washiriki waliongia tano bora.
Majaji wa shindano hilo kutoka kushoto ni Gymkhana Hilal kutoka Paka Wear , Asia Idarous na Martine Kadinda.
Unique Model Talent of the year 2012 Vestina Charles akionyesha uwezowake wa kucheza jukwaani.
Wakitumbuiza mashabiki mapema kabla ya kuingia kuonyesha mavazi ya aina mbalimbali.
Washiriki 12 wa shindano hilo wakiwa wamejipanga tayari kusubiri kutangazwa mshindi.




Na Mwandishi Wetu
FAINALI za shindano la kumsaka mwanamitindo mwenye sifa za kipekee ‘Unique Model’ 2012, limemalizika usiku wa kuamkia leo huku Catherine Masumbigana akishinda taji hilo lililofanyika kwa mara ya kwanza ndani ya ukumbi wa New Maisha Club, Oysterbay, jijini Dar es Salaam.

Shindano hilo lililokuwa likiwaniwa na warembo 12,  ambao waliweza kuonesha mavazi mbalimbali  ikiwemo ya ubunifu, usiku na mengineyo warembo hao  pia waliweza kukonga nyoyo kwa kuonesha uwezo wao wa kuimba na kucheza.

Majaji wa shindano hilo, Gymkhana Hilal, Martin Kadinda na chifu jaji,  Asia Idarous walikuwa kwenye wakati mgumu kuchagua mshindi kutokana na warembo wote kuwa na sifa za juu ambao baadaye walichuja na kubakisha watano kabla ya kubaki watatu.

Chifu Jaji wa shindano hilo, Asia Idarous ndiye alimtaja Catherine Masumbigana kuwa ndiye mshindi na kuufanya ukumbi kulipuka kwa shangwe za wapenzi na mashabiki waliokuwa wamefurika ukumbini huku nafasi ya pili ikienda kwa
Cesilia Michael na Amina Ayubu akiwa wa tatu.
Mbali ya washindi hao, pia taji la  Unique Model Photogenic  lilinyakuliwa na Elizabeth Pertty  huku Unique Model Talent litwaliwa na Vestina Charles.

Awali, akizungumza  muda mfupi kabla ya kuanza fainali hiyo, Mkurugenzi wa Unique Entertainment inayoratibu shindano hilo, Methuselah Magese aliwashukuru wadau mbalimbali  kwa kufanikisha shindano hilo mpaka hapo lilipofikia.

“Nashukuru sana wadhamini wa shindano hili kwa kutuunga mkono mara kwa mara, na tutaendelea kuleta mambo makubwa zaidi katika tasnia ya mitindo na urembo nchini” alisema Magese.

Wahiriki walioshiriki shindano hilo wengine ni Janecy Maluli, Judith Sangu, Darling Godfrey, Lulu Mramba,  Sadory Kendra, Elizabeth Borniface na Zeenarth Habib ambao hawakufaniiwa kunyakua nafasi youyote.
Fainali hizo zilizodhaminiwa na makampuni mbalimbali, zilisindikizwa na burudani kutoka kwa wanamuziki mahiri waliokuwa kivutio kingine ukumbini hapo kwa kila mmoja.

Wadhamini wa fainali hiyo walikuwa Free Media Ltd wachapishaji wa magazeti ya Tanzania Daima na Sayari, Giraffe Ocean View, Kitwe General Traders, Sophanaa Investment, Dtv, Clouds Fm, gazeti la Kiu, Mashujaa Investment Ltd, Blogu za Michuzi, Jiachie, Mtaa kwa Mtaa, Unique Entertainment, Lamada Apartments & Hotel, Fabak Fashions, Genesis Health Center na Yungdon Records, Paka Wear na Mtoko Design.

No comments:

Post a Comment