Wednesday, December 19, 2012

RATIBA YA MECHI ZA ROBO FAINALI, NUSU FAINALI NA FAINALI YA UHAI CUP 2012

Uwanja unaomilikiwa na club ya Azam Fc Chamazi Mbagala Dar es salaam.

Robo fainali za michuano ya Uhai Cup inayoshirikisha timu za vijana chuni ya umri wa miaka 10 za klabu za ligi kuu Vodacom Tanzania bara zinachezwa december 19 2012 kwenye viwanja vya Karume na Chamazi Dar es salaam.

Mtibwa Sugari inakipiga na African Lyon kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Karume saa mbili kamili asubuhi ambapo Azam na Jkt Ruvu wanacheza kwenye uwanja wa Chamazi saa mbili asubuhi pia.

Mechi nyingine ya robo fainali itakua kati ya Jkt Oljoro na Simba ambayo itachezwa saa tisa kamili alasiri uwanja wa kumbukumbu ya Karume, Coastal Union na Ruvu Shooting wanacheza Chamazi Mbagala saa kumi jioni.

Kingine muhimu cha kukufahamisha ni kwamba Nusu fainali ya Uhai Cup itachezwa ijumaa december 21 Chamazi wakati fainali na mechi ya kutafuta mshindi wa tatu zitachezwa jumapili december 23 kwenye uwanja wa Karume.(kwa hisani ya millardayo.com)

No comments:

Post a Comment