Monday, November 5, 2012

.
Kuhusu ishu ya dawa feki za ARV Naibu Waziri wa Afya na ustawi wa jamii Dr  Seif Suleiman Rashid amesema uchunguzi umeonyesha kwamba hizo dawa zilipokelewa na bohari kuu ya dawa (MSD) kutoka kiwanda cha Tanzania Phamacetical (TPI) cha Arusha.
Baada ya huo uchunguzi serikali imekifungia hicho kiwanda kuzalisha na kusambaza dawa aina zote pamoja na kuwasimamisha kazi watendaji wakuu wa MSD akiwemo Mkurugenzi, Meneja udhibiti ubora na afisa udhibiti na uchunguzi unaendelea na kwamba dawa za ARV zinazopatikana kwa sasa ni halisi hivyo ziendelee kutumika.

No comments:

Post a Comment