Thursday, November 1, 2012

SIMBA NA LIGI KUU:
Simba ambao ni mabingwa watetezi  wa ligi kuu Tanzania bara wameendelea kuokota pointi moja moja katika michezo ya nje ya Dar es salaam baada ya october 31 2012 kulazimishwa sare ya 1-1 kwenye mechi na Polisi Morogoro ambao wanaburuza mkia kwenye msimamo wa ligi kuu.
Kutokana na matokeo hayo Simba na Yanga wana pointi 23 kila mmoja sasa hivi hivyo wanatofautiana kwa magoli ya kufunga na kufungwa huku kila timu ikiwa imeingia uwanjani mara 11.

IDADI YA VITUO VYA MAFUTA VINAVYOFANYA  KAZI MBEYA KWA SASA KUTOKANA NA UHABA.
Mwandishi wa habari Joseph Mwaisango kutoka Mbeya ameripoti kwamba upatikanaji wa mafuta kwa siku hizi mbili tatu 87.8 umekua wa tabu, ni vituo vitatu tu vya kuuza mafuta vinavyouza mafuta kwa sasa ambavyo ni kwa Mama John, Mwanjelwa na katikati ya Forest mpya ambapo kuna foleni kubwa sana, bei ya mafuta ni ileile isipokua walanguzi ndio wanauza lita moja kwa elfu 5.

MOJAWAPO YA HATUA ZINAZOCHUKULIWA NA SERIKALI KUZUIA AJALI ZA MAJINI.
Kutoka bungeni Dodoma 104.4 ni kwamba Waziri wa uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe amesema Serikali imechukua hatua kadhaa kuzuia ajali za kwenye maji ambazo zimepoteza maisha ya watanzania wengi kwenye ajali zilizopita ambapo mawapo ya hizo hatua ni kuacha kusajili meli zenye umri wa zaidi ya miaka 15.
Pia Serikali imeahidi kuwasilisha bungeni muswada wa sheria ya utafutaji na uokoaji wa majini na angani ili kuhakikisha shughuli za uokoaji zinafanyika kwa kuzingatia sheria wakati ajali zinapotokea.

No comments:

Post a Comment