Monday, November 5, 2012

(Picha kutoka shaffihdauda.com)
Mashabiki wa Simba novemba 5, 2012 waliandamana mpaka kwenye makao makuu ya club hiyo Msimbazi Kariakoo Dar es salaam wakiwa na mabango mbalimbali yanayomaanisha wamechoka na ishu mbalimbali za club hiyo.

Mabango mengine yalisomeka kwamba mamluki wajirekebishe Simba mmeikuta, mengine Ndugu Kaburu kocha wetu Milovan mchango wake mkubwa bado tunamuhitaji, Kaseja tuachie timu yetu.

Hiyo yote imetokana na Simba kufungwa 2-0 na Mtibwa Sugar novemba 4 2012 Morogoro.

BAADA ya kichapo hicho msimamo wa ligi kwa timu kongwe jijini Dar es Salaam, YANGA SC imepanda kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya kuifunga Azam FC mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Ushindi huo, unaifanya Yanga iongoze Ligi Kuu kwa kufikisha pointi 26, ikiwa imebakiza mechi moja ya mzunguko wa kwanza dhidi ya Caostal Union mjini Tanga, ikifuatiwa na Simba SC yenye pointi 23, ambayo  imefungwa 2-0 na Mtibwa Sugar mjini Morogoro.

Mchezaji wa zamani  wa Ghana na klabu ya Olympique Marseille ya Ufaransa, Abedi Pele, leo ni siku ya birthday yake ametimiza miaka (48).

Mchezaji huyo amekuja nchini kufanya ziara ya kuangalia miradi mbalimbali ya kimaendeleo ya soka la Tanzania.

Pele, ambaye aliiongoza Marseille kutwaa ubingwa wa Ulaya mwaka 1992 akifunga moja ya mabao dhidi ya AC Milan ya Italia mwenye watoto wawili wanaocheza mpira ambao ni Jodan na Dede wanachezea Olimpic Marseille ya Ufaransa.

No comments:

Post a Comment