Saturday, November 24, 2012

MWAKYEMBE AWATUNUKU STASHAHADA ZA KAWAIDA,STASHAHADA ZA JUU NA SHAHADA MBALIMBALI WANAFUNZI WA CHUO CHA USAFIRISHAJI(NIT)

 Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe(Kulia kwa Mkuu wa Chuo), akisikiliza maelezo ya maendeleo ya Jengo Jipya la Chuo Cha Usafirishaji(NIT) kutoka kwa Mkuu wa Chuo hicho, Mhandisi.Dkt. Zacharia Mganilwa (aliyevaa suti ya Kaki), wakati Waziri wa Uchukuzi alipotembelea Chuoni hapo Leo Mchana kutunuku Stashahada za Juu, Stashahada za Kawaida na Shahada mbalimbali katika mahafali ya 28 ya Chuo hicho.
Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji(NIT), Mhandisi, Dkt. Zacharia Mganilwa(aliyevaa suti ya Kaki), akimuonyesha Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe(Kulia kwa Mkuu wa Chuo), eneo ambalo Chuo kimelitenga kwa ajili ya wenye Magari watakaomua kupaki magari yao na kwenda kutumia Usafiri wa Treni inayotoka Ubungo kuelekea Stesheni jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji(NIT), Mhandisi.Dkt. Zacharia Mganilwa(aliyevaa suti ya Kaki), akimueleza Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe(Kulia kwa Mkuu wa Chuo), namna ambavyo Maktaba ya Chuo hicho inavyofanya kazi, chuoni hapo Leo Mchana. Dk Mwamkyembe alipita katika maeneo mbalimbali kabla ya kuhudhuria mahafali ya 28 ya Chuoni hapo.

Baadhi ya Wageni walioalikwa katika mahafali ya 28 ya Chuo cha Usafirishaji(NIT), wakimsikiliza Mgeni Rasmi Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe leo mchana katika Viwanja vya Chuo hicho.
Waziri wa Uchukuzi,Dk. Harrison Mwakyembe akihutubia wahitimu pamoja na Wageni waalikwa katika mahafali ya 28 ya Chuo cha Usafirishaji(NIT), Mahafali hayo yamefanyika katika Viwanja vya Chuo hicho Leo Mchana, ambapo wahitimu wa Kozi mbalimbali wametunukiwa Stashahada za Kawada, Stashahada za Juu na Shahada.



Waziri wa Uchukuzi.Dk. Harrison Mwakyembe(Aliyevaa kofia Nyekundu),akiwa katika picha ya pamoja na Wahitimu wa kozi mbalimbali kutoka  katika Chuo Cha Usafirirshaji(NIT),jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment