Umuhimu wa Urafiki katika mahusiano..
Urafiki katika Mahusiano.
Hebu tutafakari mahusiano ya muda mrefu au mahusiano yanayopelekea
ndoa!
Kama mnapenda mapenzi yenu yadumu hadi pale “kifo
kitakapo watenganisha”, basi ni bora kuhakikisha kwamba mahusiano ama mapenzi
yenu yamejengwa katika msingi mkuu na imara ambao ni – URAFIKI.
URAFIKI ni msingi muhimu katika kutengeneza mahusiano imara na yenye
mafanikio. Bila urafiki hamna lolote. Mambo mengine ni ya muhimu pia
katika mahusiano, bila ya shaka, lakini
unahitaji ya ziada ili kuweza
kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika maisha ya mahusiano
ambazo hakuna mtu ambaye anaweza kuzikwepa.
Kama mtu binafsi unapaswa kuboresha uwezo wako binafsi pale
inapokuja suala la mahusiano. Badala ya kuangalia zaidi upande wa pili wa kutafuta
mshirika wa mahusiano ni vyema zaidi ukatumia muda mwingi kutafakari ni aina
gani ya mtu ambaye unatarajia kujenga naye urafiki. Kujenga urafiki ndiyo hasa mwanzo
wa mahusiano. Ni kushirikiana zaidi kwa kufahamiana, kujuana, kufahamu
malengo yenu katika maisha, thamani yenu na yale ambayo kila mmoja wenu
anayapendelea ama hapendezwi nayo. Pamoja na mambo mengine mengi mazuri ambayo
yatawafanya kuwa wa pekee.
Kuna muda wa kutosha sana katika maisha ya mahusiano kwa ajili ya
mapenzi na kujitoa kwa mwenzako, hakuna haja ya kukimbilia hayo!
Ni kweli kwamba kadiri unavyo ahirisha kujiingiza katika
mapenzi na kujenga urafiki, ndivyo jinsi ambavyo utaweza kujenga mahusiano
yaliyo bora na mwenzi wako wa baadaye katika maisha. Kwa mwenendo huo
mtajifunza na kuona kama mnaendana na mko tayari kila mmoja kwa mwenzake.
Hivyo basi kama itakuwa hamuendani ama mmoja hayuko tayari kwa
mahusiano hayo ni rahisi kuachana huku kila mtu akiwa na utu wake kama
mlivyokutana!
Kujenga msingi imara ni muhimu, mara baada ya kuujenga ni
rahisi kuendelea kutengeneza maisha na mahusiano mazuri juu ya msingi huo. Chukua
muda, fahamianeni, jengeni urafiki ambao mtaweza kuuenzi kwa muda wa miaka
mingi katika maisha yenu na hatimaye kuweza kuwa na maisha bora ya
mahusiano yenye mafanikio na faida kwa maisha ya pande zote husika.
dada yangu asante sana kwa ushauri huu hakika umenisaidia sana hasa katika kuwa na malengo nimekuwa na marafiki wengi ila hakuna hata mmoja nilieweza kuwa na malengo naye sasa naanza upya asante /fabian
ReplyDelete