DIAMOND PLATNUM AINGIA MKATABA NA I-VIEW MEDIA
Mkurugenzi wa kampuni ya I-View Studios, Raqey Mohammed akibadilishana
mkataba na Msanii Diamond Platnumz baada ya kusaini. Wanaoshuhudia ni
Mwanasheria wa Diamond, Paul Mgaya, Mwanasheria wa I-View Dr. Peter
Aringo na Mkurugenzi wa One Touch Solutions, Petter Mwendapole.
Mkurugenzi wa Kampuni ya I-View Studios, Raqey Mohammed ( kushoto) na
msanii Diamond Platnumz wakisaini mkataba wa kufanya kazi pamoja. Wanaoshuhudia ni
Mwanasheria wa Diamond, Paul Mgaya, Mwanasheria wa I-View Dr. Peter
Aringo na Mkurugenzi wa One Touch Solutions, Petter Mwendapole
MSANII wa kimataifa wa Tanzania, Naseeb Abdul
‘Diamond Platnumz’ ameingia mkataba na kampuni ya I-View Studios ili
wasimamie kazi zote kwa muda wa miaka miwili.
Mkurugenzi wa kampuni ya One Touch Solution ya
mjini Dar es Salaam, Petter Mwendapole amesema I-View itasimamia mikataba yote
ya kazi zote za msanii huyo na yeyote atakayetaka kufanya kazi na Diamond kwa
sasa itabidi awasiliane I-View.
“Diamond ameamua kufanya kazi zake kimataifa, na
ameingia mkataba na I-View ambapo wao ndio watakuwa wakisimamia maonyesho,
matangazo, nyimbo kwenye simu, nguo kila kitu ambacho kinahusiana naye
kinapaswa kupitia I-View,” amesema.
Mwendapole alisema pamoja na maonyesho, lakini I-View
pia itawajibika katika muonekano mpya wa msanii huyo ambaye kwa sasa anatamba
ndani na nje ya Tanzania. One Touch Solutions ndio watakuwa wasemaji wa msanii
huyo.
Diamond kwa upande wake alisema anataka kufungua
ukurasa upya katika tasnia ya muziki nchini na kwa anaamini utasaidia katika kumfanya
aongeze nguvu zaidi katika kutunga na kutengeneza nyimbo zake.
“Hii yote ni kuhakikisha nafanya kazi zangu kwa
ufanisi badala ya kujirundikia mambo mengi, kuna watu walikuwa wakinitafuta
wanashindwa kunipata lakini sasa watakuwa wanafahamu ofisi ziko wapi na
wanawasiliana na menejimenti inawapa majibu, watu wa habari watakuwa na mtu wa
kuwasiliana nae moja kwa moja hata kama sipatikani,” amesema.
Diamond anatarajia kutoa wimbo wake mpya ambao pia
utarekodiwa na kampuni ya I-View. Tayari usaili umeshafanyika kwa ajili ya
wale ambao wataonekana kwenye video hiyo.
I-View mbali na kazi kupiga picha, lakini pia
inatengeneza matangazo mbalimbali ya TV, Radio, mabango, ubunifu wa kazi
mbalimbali za sanaa.
No comments:
Post a Comment