ASIA IDARIOUS KUSHIRIKI ABAYA FASHION SHOW
MBUNIFU mkongwe nchini, Asia Idarious atashiriki katika onyesho
la kipekee lililobatizwa jina la Abaya Fashion Show and Luncheon
litakalofanyika Oktoba 12 ambalo litakuwa maalumu kwa wanawake tu.
Idarious
anasema baada ya kufanya maonyesho ya mengi huko Marekani safari hii
atashiriki katika onyesho hilo la kipekee kuonyesha ukongwe wake katika
fani hii.
"Kwa miongo mitatu niliyokuwemo ndani ya fani hii
naweza kusema nimejifunza mambo mengi nilipokuwa Marekani, nilifanya
'fashion show' katika miji mbalimbali ambayo kwa kweli imenijenga na
ujuzi wake sasa nitauonyesha siku hiyo," anasema Asia.
Asia
anasema kuwa hii itakuwa mara ya kwanza kwake kufanya onyesho la aina
hii, lakini kutokana na uzoefu alionao anasema anaamini litakuwa bora.
"Mimi
ni mbunifu mkongwe kuliko wote, nimeshafanya shoo ambazo huwezi
kuzihesabu, Abaya itakuwa ya aina yake kwani kutokana na mpangilio mzima
wa tukio lenyewe," anasema Asia.
Mwenyewe anasema anajivunia kwa kuweza kufanya maonyesho makubwa nchini ikiwemo Lady in Red na Khanga ya Kale.
Onyesho
hilo linalodhaminiwa na Red Onion, An Nisa na Valley Spring litafanyika
katika mgahawa wa Red Onion uliopo katika jengo la Haidery Plazer
jijini Dar.
Tukio hilo la aina yake lililopewa jina la Abaya
Fashion Show Luncheon litafanyika kwa muda wa saa tatu tu, kuanzia saa
tisa na nusu mchana mpaka saa kumi na mbili.
Mbali na Asia
mbunifu mwingine nguli, Mustafa Hassanali naye ataonyesha Abaya zake
ambazo mapema mwaka huu alizionyesha huko Dakar, Senegal.
Kwa kuwa sherehe hii ni maalum kwa wanawake tu, Mustafa atawakilishwa na mwanamke katika onyesho hilo.
Aidha
mmiliki wa lebo ya Kidoti, Jokate Mwegelo atakuwa mshereheshaji huku
wanamitindo mahiri kama Fiderine Iranga na Warda Walid wakiwa miongoni
mwa watakaaonyesha mavazi hayo siku hiyo.
No comments:
Post a Comment