IGP MWEMA MGENI RASMI KATIKA KUFUNGA MAFUNZO YA POLISI ZANZIBAR
Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi Zanzibar
Mkuu wa
Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali Saidi Mwema, Ijumaa na Jumamosi
wiki hii, atakuwa mgeni Rasmi katika sherehe za kufunga mafunzo ya
uongozi mdogo kwenye Chuo cha Taaluma ya Polisi Zanzibar.
Taarifa ya Mkuu wa Chuo cha
Polisi Zanzibar (Zanzibar Police Academy) SSP Raamadhani Mungi, imesema
kuwa mafunzo hayo ya mwezi mmoja yatafungwa katika awamu mbili tofauti.
Amesema awamu ya kwanza, mafunzo
hayo itafanyika katika chuo cha Mafaafisa wa Mafunzo (Magereza)
kilichopo eneo la Hanyengwa mkoa wa Kusini Unguja ambapo yatafanyika
maonyesho ya utayari na Medani za kivita.
Kamanda Mungi amesema maonyesho
hayo yatanza saa 9.00 Arasili siku ya Ijumaa Oktoba 5, mwaka huu, kwa
kuwashirikisha Wahitimu wa vyeo vya RSM na Staf Sajent waliokuwa
wakishiriki katika mafunzo hayo.
Amesema sherehe hizo zitafuatiwa
na zile zitakazofanyika kwenye Viwanja vya Polisi Ziwani mjini Mjini
Zanzibar zitakazoanza saa 2.30 asubuhi siku ya Jumamosi Oktoba 6, 2012.
Kamanda Mungi amesema siku hiyo
asubuhi, IGP Mwema, atakagua gwaride kabla ya gwaride hilo kupita mbele
yake kwa mwendo wa pole na mwendo wa waharaka kwa heshma.
Kamanda Mungi ametoa wito kwa
wananchi wa vijiji vya Jendele, Ndigani, Cheju, Kwaka, Tunguu, Dunga na
wenyeji Hanyegwa pamoja na wakazi wa mjini Zanzibara na Viunga vyake,
kufika kwa wingi katika Chuo hicho cha Hanyegwa na Ziwani ili kujionea
maonyesho mbalimbali.
Zaidi ya Askari 920 kutoka katika
mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Visiwani waliokuwa wakihudhuria
mafunzo ya Sajenti, Staf Sajent na RSM watahitimu mafunzo yao na
kutunukiwa vyeo vipya.
No comments:
Post a Comment