Stori kubwa Kenya ambayo imeshika nafasi ya kwanza
ni kuhusu mamlaka ya mawasiliano nchini Kenya kuzizima kiteknolojia simu
zote zilizofeki ambazo zimekuwa zikitumiwa na wakenya.
Mtangazaji wa Citizen Tv/Radio
William Tuva ameripoti kwamba wakenya walionunua simu feki wapo kwenye
wakati mgumu na itawabidi wanunue simu original kwa sasa ili kurudi tena
kwenye mawasiliano.
Ameripoti pia kwamba
inasemekana katika mtandao wa simu za mkononi wa Safaricom peke yake ni
wateja laki sita ambao wameripotiwa simu zao kuzimwa kwa sababu ni feki.
Kwenye line nyingine Tuva
ameripoti pia kwamba Kenya imepoteza mabilioni ya shilingi kutokana na
simu feki ambazo zimekua zikiingia sokoni kwa njia ambayo siyo halali.
Baadhi ya wananchi ambao simu
zao zimefungwa wamekaririwa wakisema waliamka asubuhi na kukuta simu zao
hazifanyi kazi, kumbe tayari zimeshazimwa kiteknolojia na tume ya
mawasiliano nchini humo ambapo kwa mujibu wa BBC n wateja milioni mbili
na nusu ambao simu zao zimezimwa.
Mmoja wa watu hao amekaririwa
akisema “usiku ninawekaga alamu nataka saa 11 niamke, sikusikia naamka
tu naona nje kunapambazuka na simu yangu wamezima’
No comments:
Post a Comment