Wednesday, October 3, 2012

PICHA ZA UZINDUZI WA MAISHA PLUS 2012

  Masoud DSC_7231 (800x537) (2) DSC_7231 (800x537) DSC_7232 (800x537) (2) DSC_7232 (800x537) DSC_7233 (800x537) (2) DSC_7233 (800x537) DSC_7234 (800x537) (2) DSC_7235 (800x537) (2) DSC_7236 (800x537) DSC_7243 (800x537) (2) Mratibu wa shindano la Maisha Plus/ Mama Shujaa wa Chakula 2012, Masoud Kipanya akiongea na waandishi wa habari DSC_7250 (800x537) (2) DSC_7263 (800x537) (2) DSC_7263 (800x537) Nyumba watakazokuwa wanakaa Mama Shujaa DSC_7268 (800x537) DSC_7269 (800x537) (2) DSC_7269 (800x537) Masoud Kipanya akimtembeza Mheshimiwa Ummy Mwalimu kwenye kijiji DSC_7275 (800x537) DSC_7276 (800x537) (2) DSC_7276 (800x537) DSC_7278 (800x537) (2) DSC_7280 (800x537) Mwanamuziki Keyshia akihojiwa na mwandishi wa habari DSC_7292 (800x537) DSC_7302 (800x537) Mheshimiwa Adam Malima akiteta jambo na mkurugenzi mkazi wa OXFAM, Monica Gorman Burudani ya kundi la akinamama DSC_7311 (800x537) 
Naibu Waziri wa Chakula na Ushirika, Adam Malima na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu, jana wamezindua shindano la Maisha Plus/Mama Shujaa wa Chakula 2012.

Uzinduzi huo umeshuhudia wanawake 14 waliongia kambini kwenye kijiji cha Maisha Plus ambao baadaye wataungana na vijana watakaoshiriki kwenye shindano la Maisha Plus.

Akizungumza baada ya kuwatambulisha Mama Shujaa 14 watakaoshiriki kwenye shindano hilo kumpata mshindi mmoja, Mheshimiwa Malima alisema serikali itahakikisha kuwa mwanamke ambaye ni mzalishaji mkuu wa chakula kwenye jamii ya Tanzania anawekewa mazingira mazuri ambayo yatasaidia shughuli za kilimo ziwe na tija zaidi.

Kwa upande wake Mheshimiwa Mwalimu alisema wanawake wamekuwa wakikumbwa na changamoto nyingi kwenye jamii ambapo pamoja na kushiriki katika uzalishaji wa chakula wamekua wakikosa mamlaka na uamuzi wa kile wanachokitayarisha kutokana na kuendelea kuwepo kwa mfumo dume ambapo mwanaume huwa juu ya mwanamke.

Alisema wanatambua kuwa kipato kinachopatikana kutokana na shughuli za kilimo kinamilikiwa na wanaume ambapo pia wanawake wengi hawamiliki ardhi.

Aliongeza kuwa serikali inazitambua changamoto hizo na inafanya kazi kuziondoa kabisa.

Mheshimiwa Mwalimu alisisitiza kuwa shindano la Mama Shujaa lengo lake ni kuikumbusha jamii umuhimu wa mwanamke katika uzalishaji wa chakula na kwamba sheria inasema mwanamke na mwanaume wana haki ya sawa katika maamuzi ya kile wanachozalisha.

Naye Mkurugenzi mkazi wa shirika la OXFAM ambalo ni wadhamini wa shindano hilo Bi. Monica Gorman alisema wanawake ni waendeshaji wa uchumi wa Tanzania lakini umuhimu wao umefunikwa kwa muda mrefu hivyo kwa kutumia shindano la Mama Shujaa wa Chakula, wanawake wanamulikwa ili wapate kile wanachostahili.

Shindano hilo lina lengo la kuwainua wanawake, kuwapa moyo na kuwaunga mkono wakulima wadogo wanawake nchini na kuongeza kukubalika kwa mchango wao katika kilimo.

Uzinduzi wa Maisha Plus/Mama Shujaa wa Chakula 2012 ulioneshwa live kupitia kituo cha TBC1.

No comments:

Post a Comment