AIRTEL YATEMBELEA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUMU WA UHURU MCHANGANYIKO
Afisa uhusiano na matukio wa Airtel Dangio Kaniki
akiwapatia chai watoto shule ya Uhuru Mchanganyiko wakati Airtel
ilipotembelea shule hiyo itakayofaidika na mpango maalumu wa Airtel
kwa kushirikiana na BAMVITA wenye lengo la kuchangia vitabu kwa watoto
wenye mahitaji maalum . Airtel imeanza kutembelea shule zilizopo Dar es
Salaam pamoja na mikoani na kubainisha matatizo wanayokumbana nayo ili
kuona namna ya kuwasaidia watoto hao wenye mahitaji maalum.
Airtel Communication and event officer Dangio
Kaniki serve breakfast to Uhuru Mchanganyiko children during Airtel
visit to school yesterday; the school is one of the beneficiaries of the
project launched by Airtel in partnership with BAMVITA aiming to
facilitate teaching aids to students with special needs. Airtel has
started visiting school in Dar and upcountry to realize their need and
mobilize funds to support children with special needs.
Meneja huduma za jamii wa Airtel Hawa Batuli
(katikati)akiongea na mwalimu mkuu wa shule ya Uhuru Mchanganyiko Anna
Mang'enya wakati Airtel ilipotembelea shuleni hapo jana. Airtel imeanza
kutembelea shule zilizopo Dar es Salaam pamoja na mikoani na kubainisha
matatizo wanayokumbana nayo ili kuona namna ya kuwasaidia watoto hao
wenye mahitaji maalum. Kushoto ni Afisa uhusiano na matukio wa Airtel
Dangio Kaniki.
Airtel Social Responsibility Manager Hawa
Batuli(middle) speaks to Uhuru Mchanganyiko school Head teacher during
Airtel visit to the school, Airtel has started visiting school in Dar
and upcountry to realize their need and mobilize funds to support
children with special needs. On the left is Airtel Communication and
event officer Dangio Kaniki
Afisa uhusiano na matukio wa Airtel Dangio Kaniki
akinywa chai pamoja na watoto wa shule ya Uhuru Mchanganyiko wakati
Airtel ilipotembelea shule hiyo itakayofaidika na mpango maalumu wa
Airtel kwa kushirikiana na BAMVITA wenye lengo la kuchangia vitabu kwa
watoto wenye mahitaji maalum . Airtel imeanza kutembelea shule zilizopo
Dar es Salaam pamoja na mikoani na kubainisha matatizo wanayokumbana
nayo ili kuona namna ya kuwasaidia watoto hao wenye mahitaji maalum.
Airtel Communication and event officer Dangio
Kaniki having breakfast with Uhuru Mchanganyiko children during Airtel
visit to the school yesterday; the school is one of the beneficiaries of
the project launched by Airtel in partnership with BAMVITA aiming to
facilitate teaching aids to students with special needs. Airtel has
started visiting school in Dar and upcountry to realize their need and
mobilize funds to support children with special needs.
Meneja huduma za jamii wa Airtel Hawa Batuli
(kushoto) akimshukurua mwalimu mkuu wa shule ya Uhuru Mchanganyiko Anna
Mang'enya kwa kuwapokea walipotembelea shule hapo ambapo Airtel imeanza
kutembelea shule zilizopo Dar es Salaam pamoja na mikoani na kubainisha
matatizo wanayokumbana nayo ili kuona namna ya kuwasaidia watoto hao
wenye mahitaji maalum. Kushoto ni Afisa uhusiano na matukio wa Airtel
Dangio Kaniki .Airtel Social Responsibility Manager Hawa
Batuli(middle) shake hands thanking Uhuru Mchanganyiko school Head
teacher for hosting Airtel visit to the school, Airtel has started
visiting school in Dar and upcountry to realize their need and mobilize
funds to support children with special needs. On the left is Airtel
Communication and event officer Dangio Kaniki.
Kampuni ya simu za
mkononi ya Airtel imewahimiza watanzania kuendelea kuchangia katika
mradi wa kuchangia vifaa kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalum
unaoendeshwa na Kampuni ya Airtel kwa kushirikiana na Baraza la
maendeleo ya vitabu Tanzania (Bamvita)
Afisa uhusiano na
matukio wa Airtel Dangio Kaniki amesema kampuni hiyo ikiwa na Balozi
wake, AY imeanza kutembelea shule zilizopo Dar es Salaam pamoja na
mikoani na kubainisha matatizo wanayokumbana nayo ili kuona namna ya
kuwasaidia watoto hao wenye mahitaji maalum. Airtel inaamini kwamba
watoto hao wenye mahitaji maalum wakiwezeshwa kielimu wataweza kutimiza
ndoto zao na kuchangia katika maendeleo ya kiuchumi nchini.
Akiongea wakati
walipotembelea shuleni hapo Meneja huduma kwa jamii Hawa Bayumi alisema ”
Ni matumaini yetu kuwa watanzania na wale wasio watanzania kwa ujumla
wataendelea kutuunga mkono ili kuweza kutimiza lengo hili la awali na
kisha kuongeza shule za mikoani mara baada ya kukamilisha mahitaji haya
katika shule hizi za Dar es Salaam. Kampeni hii itaendeshwa kwa muda wa
miezi mitatu , na watanzania wanaweza kuchangia kwa kutuma neno “Vitabu” kwenda namba 15626 na utakuwa umechangia shilingi 200 katika mradi huu au kupitia Airtel Money unapiga *150*60#
ingiza jina la biashara VITABU na kuchangia kiwango chochote kile.
Tunachukua fulsa hii kuwaomba watanzania wote kuchangia ili kuwafikia
watoto wengi zaidi nchin”
Nae Mwalimu Mkuu wa
shule ya Uhuru Mchanganyiko Anna Mang'enya amesema “shule hiyo
inakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo uhaba wa vifaa vya
kufundishia. bila vifaa hivyo maalum itakuwa vigumu kwa wanafunzi
kutimiza ndoto zao zakuendelea kielimu”.
Aidha Ameishukuru Airtel
na BAMVITA kwa kuweza kuanzisha mradi huu na kuweza kuwahamasisha
watanzania kuchangia ili waweze kupata vitendea kazi na kuongeza kuwa
shule hiyo bado inakabiliwa na changamoto nyingi katika elimu hivyo
kuiomba kampuni hiyo kuendelea kuisaidia katika mambo mengine.
Zena Yahaya Mwanafunzi
Uhuru Mchanganyiko alikuwa na haya ya kuongeza “tunawashukuru Airtel
kwa kuja kututembelea leo, tunawaomba watanzania wote waendelee
kutusaidia kwa kushirikiana na Airtel katika mradi huu wa Vitabu ili
kuweza kutusaidia katika kununua vifaa vya kutusaidia hapa shuleni na
kuhakikisha tunapata elimu bora.”
Airtel inatambua umuhimu
wa Elimu na tunaamini Tanzania itajengwa na sisi wenyewe hivyo basi
lengo la mradi huu ni kutoa nafasi kwa jamii yetu kuweza kuchangia
elimu ya msingi kwa watoto wenye mahitaji maalum kwa kuwanunulia vitabu
na nyenzo za walimu kufundishia. Kwa kuanzia tumeanza kutembelea shule
mbili za jijinini Dar es Salaam zitafaidika na mpango huu ambazo ni
Sinza Maalum, Uhuru Mchanganyiko ikifuatiwa na Buguruni Viziw.
No comments:
Post a Comment