KAMPUNI YA GREEN WASTE PRO YALALAMIKIA UJENZI USIOFUATA TARATIBU KUCHAFUA MAZINGIRA YA MJI.
Malori
yanayobeba Udongo katika eneo hilo la Ujenzi yakiingia na kutoka wakati
wa usiku huku yakiwa hayjafunikwa na maturubai hali inayosababisha
kumwaga udongo katika barabara za jiji na kusababisha uchafuzi
unaolalamikiwa na kampuni zinazofanya usafi.
Bango
la Mkandarasi anayejenga jengo hilo lililopo kwenye kiwanja namba 01
katika makutano ya Barabara ya Ali Hassan Mwinyi na Ufukoni jijini Dar
es Salaam ambapo linaonyesha Wajenzi ni Kampuni ya China Railway
Jiachang Engineering Co. Ltd.
Moja ya Malori ya mchanga likitoka baada ya kuzoa udongo katika jengo hilo na kujazwa kupita kiasi.
Muonekano
wa uchafu katika barabara kutokana na kumwagika kwa udongo unaozombwa
na malori hayo ambao unapelekea kuzibisha mitaro na kuchakaza lami.
Malori yakiwa kwenye foleni ya kuzoa udongo katika jengo hilo.
Tunapozungumzia Suala la usafi asilimia kubwa ya wanajamii wanaelewa maana yake na umuhimu wake.
Na
tunapozungumzia kutunza usafi katika mazingira yetu tunamaanisha kuanzia
tunapoishi hadi katika barabara za ndani na zile kubwa za lami
zinazotumika mijini.
Wote
tumeshuhudia Manispaa ya Ilala ambayo ndio kitovu cha jiji la Dar es
Salaam ikizindua kampeni za kufanya usafi katika maeneo yote ikimo
katika barabara kubwa za jijini.
Katika kutimiza malengo hayo kampuni ya ‘Green Waste Pro Ltd’ ikafanikiwa kushinda zabuni ya kufanya usafi katika manispaa hiyo.
Ama kwa
hakika kapuni hiyo yenye magari yakutosha likiwemo gari la kisasa la
kupiga deki barabarani ikaanza kazi hiyo na kipindi kifupi matokeo
yakaaanza kuonekana.
Sasa
basi katika kile kinachoonekana kama ama kutojali au kupuuzia taratibu
za usafi kampuni moja iliyopewa kandarasi ya kujenga jengo moja katika
ene la mtaa wa Ufukweni jiji Dar imekuwa ikichafua mazangira ya jiji
bila kujali.
Mo Blog
imeshuhudia magari makubwa ya kampuni hiyo yakibeba udongo nyakati za
usiku huku yaendeshwa hovyo na kumwa udongo huo barabarani na kuacha
vumbi likitimka hewani.
Tukizungumza na Mkurugenzi wa Kampuni ya ‘Gree Waste Pro Ltd’ Bw. Mac
Antony Shayo amesema kwa kawaida magari yanayofanya shughuli hiyo
yanapswa kusafishwa pale pale kwe saiti kabla ya kutoka nje, ili kuepuka
kuchafua mji.
Ameongeza
kusema kuwa kingine ni kwamba magari hayo yanajazwa sana udongo kuliko
kiwango kinachoshauriwa na pia hayafunikwi, hivyo yana mwaka tu matope
barabara yote kuanzia yanakotoka, na mbaya zaidi yanaingia ‘City
Centre’.
Amesema
kuwa utaratibu huo sio sahihi na gharama zinazotumika kusafisha barabara
ni kubwa na kinachojitokeza kuwa sasa tunashinda sisi tunasafisha wao
wanakazana kuchafua.
Bw.
Shayo amesema pamoja na kuchafua barabara pia ndio chanzo cha uharibifu
wa lami, na pia udongo kujaa katika mifereji kipindi cha mvua.
Aidha
amesema kampuni hiyo inapaswa inyimwe kuendelea na kazi hiyo mpaka
itakaporekebisha taratibu zao za utendaji ikiwemo kusafisha hayo magari
yao ili yaweze kubeba uchafu kwa njia ya usafi.
Afafanua
kuwa gari hizo zisijazwe na zifunikwe kama sheria inavyotaka kwa kuwa
sheria haikuwekwa ili mtu asimamiwe bali imewekwa ili itekelezwe.
No comments:
Post a Comment