Serikali kwenye mkoa wa Tanga
96.0 imesema itafanya kila linalowezekana kuhakikisha inavunja vitendo
vinavyoendelea vya mauaji ya raia kwenye mkoa huo.
Jumla ya watu 11 wameripotiwa
kuuwawa kikatili kuanzia septemba 1 mpaka septemba 28 mwaka huu kutokana
na sababu mbalimbali kama za kishirikina, sheria mikononi, wivu wa
kimapenzi na ujambazi.
Oktoba 8 mwaka huu mlinzi wa
kampuni ya Mult System ametekwa na hajulikani alipo mpaka sasa, alitekwa
wakati akiwa lindoni kwenye ofisi za halmashauri ya wilaya ya Mkinga
ambapo baada ya kutekwa majambazi yalifanikiwa kuiba gari aina ya
Landcruiser tukio ambalo lilithibitishwa na Kamanda wa polisi Tanga
Costantine Massawe.
Mkuu wa mkoa wa Tanga luteni
mstaafu Chiku Galawa amesema jeshi la polisi kwa ujumla halijashindwa
kukanbiliana na mauaji hayo ambayo amesema yanauchafulia jina mkoa wa
Tanga.
No comments:
Post a Comment