Wakati wa kumuaga Liberatus
Barlow aliyekua kamanda wa polisi mkoani Mwanza ambae aliuwawa weekend
iliyopitwa kwa kupigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi ambao
walipokutana nae walijifanya polisi wa doria, Mkurugenzi wa upelelezi wa
makosa ya jinai nchini (DCI) Robert Manumba amesema polisi wa Mwanza
wawe watulivu kwenye kipindi hiki kigumu lakini ni lazima walipe kisasi
kwa kuwakamata waliohusika.
Namkariri akisema “nawaombeni
tuendeleze utulivu lakini tuhakikishe kwamba tunalipa kisasi cha tukio
hili la kikatili kwa kuwakamata waliohusika, hatutalala tutaendelea kuwa
na ninyi na kwa kweli kama tunavyokabiliana na uhalifu wowote, auliwe
mwananchi wa kawaida, afisa, kiongozi… ni kifo lazima kishughulikiwe”
Mkuu wa mkoa wa Mwanza
Evarist Ndikilo amesema mazingira ya kuuwawa kwa Kamanda Barlow bado
hayajawa wazi, alipofika kwenye eneo alilouwawa usiku kati ya saa saba
na saa nane akasimama na kuegesha gari kama kawaida na kumteremsha huyo
dada yake, ghafla mbele yake wakajitokeza watu wawili ambapo Kamanda
alipoona kama kuna mazozo ikabidi awaulize wale jamaa akisema hamnijui?
waliporushiana maneno sana ikabidi achukue radio ili kuwasiliana na
polisi ambapo kabla ya kufanya hivyo ndio alipigwa risasi.
Namkariri mkuu wa mkoa akisema
“amepigwa risasi kutokea mlango wa abiria kwa sababu risasi imepigwa
begani na kutokea kwenye maeneo ya shingoni”
No comments:
Post a Comment