Thursday, August 2, 2012

Mwana FA na Godzilla.

July 25 2012 Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe alizungumza bungeni Dodoma na kusema “Makampuni ya simu Tanzania kwa mwaka yanapata shilingi bilioni 43 kutokana na biashara ya ringtones za nyimbo za wasanii, tulitarajia tunaponunua hizo ringtone wasanii wetu watafaidi lakini asilimia 80 ya fedha hizo inakwenda kwa kampuni ya simu alafu asilimia saba tu ndio inakwenda kwa msanii”
Siku sita baada ya hii kauli wasanii mbalimbali walioungana wakiwemo wa Bongo fleva, Gospel na Dance na kutangaza kusimamisha mikataba ya mauzo ya nyimbo zao kama ringtones kwenye makampuni ya simu.

Staa wa single ya ‘Ameen’ Mwana Fa ni miongoni mwa wasanii waliofanya hivyo pia, ambapo leo ameamplfy kwamba huwa hapendelei kutaja mapato yake hadharani lakini amekubali kutaja ili kutoa picha kamili ya kile wasanii wanachokipata kwenye mauzo ya ringtones.

Amesema hamna chochote ambacho amewahi kukifanya cha maendeleo kutokana na pesa ya mauzo ya nyimbo zake kama ringtones wakati nyimbo zake nyingi zilizohit aliziuza kama ringtone pia, na kutolea mfano Smash hit ya ‘Yalaiti’ aliyofanya na Linah ambapo kwenye mauzo ya ringtone kwenye miezi mitatu alipata shilingi kama laki tatu.

Fa alitaja pia sehemu ya list ya wasanii walioungana na kusimamisha mikataba yao ya hayo mauzo ya ringtone na makampuni ya simu kuwa ni Profesa Jay aliekua wa kwanza, Ay, Roma, Diamond Platnums, Fid Q na THT ambapo wamesimamisha hayo mauzo mpaka maamuzi ya kulipwa vizuri yatakapofanywa na makampuni ya simu.

Kwenye Press release ya kuuvunja huo mkataba, wasanii wameandika “Kwa ujumla wetu sisi Wasanii toka Tanzania tunaofanya muziki wa Gospel, Rhumba , Taarabu pamoja na Bongo fleva tumeamua kutoa agizo kwenu la kusimamisha mauzo ya kazi zetu za muziki katika mtindo wa Ringtone na Callertunes katika mitandao ya simu na kufuta mkataba tuliosaini kati yetu sisi Wasanii na Kampuni mpaka hapo tutakapokaa sisi kama wasanii, nyinyi kama wasambazaji wa muziki wetu, pamoja na Mitandao ya simu ili kuzungumzia namna mpya ya sisi na nyinyi kufanya kazi.

“Sababu ya kusimamisha na kufuta mikataba na wanaofanya biashara ya kuuza maudhui yetu ni pamoja kampuni husika kushindwa kuweka wazi taarifa za mauzo ya nyimbo pamoja na kutolipa katika muda husika kama ilivyoanishwa katika mikataba husika”

Mpaka July 31 2012 jioni ni wasanii 153 walikuwa wameshasaini barua hizo na wengine wanaendelea kusaini.

No comments:

Post a Comment