MICHUANO YA AIRTEL RISING STARS YAANZA NAIROBI
Mkurugenzi
wa Masoko wa Timu ya Manchester United,Jonathan Rigby (kulia)
akikabidhi jezi kwa Waziri Mkuu wa Kenya,Mh. Raila Odinga (kushoto)
wakati wa ufunguzi rasmi wa Mashindano ya Airtel Rising Stars kwa
Afrika yatayofanyika jijini Nairobi,Kenya.Wengine pichani ni Manoj
Kohli CEO (International) & Joint MD,Ofisa Mkuu wa Masoko wa
Bharti Airtel na Airtel Africa,Andre Beyers (wa tatu kulia).
Mkurugenzi
wa Masoko wa Timu ya Arsenal,Angus Kinnear (kushoto) akimkabidhi jezi
Waziri Mkuu wa Kenya,Mh. Raila Odinga wakati wa ufunguzi rasmi wa
Mashindano ya Airtel Rising Stars yatayofanyika jijini Nairobi,Kenya.
Michuano
ya Airtel Rising Stars barani Afrika imeanza kutimua vumbi Jijini
Nairobi, Kenya. Michuano hiyo imeleta pamoja wavulana na wasichana wenye
umri chini ya miaka kumi na saba na itaendelea mpaka Agosti 25.
Michuano
hiyo ambayo ilianzia kwenye ngazi ya wilaya mpaka Taifa na kufanyika
kwenye nchi 15 barani Afrika. Huu ni mpango kabambe wa Airtel Rising
Stars, wenye lengo la kuwapa vijana chipukizi fursa ya kuonyesha vipaji
vyao. Ikiwa ni ya moja ya michuano mikubwa kabisa barani Afrika, jumla
ya timu 18,000 zilishiriki na wachezaji 324,000 – wavulana na wasichana
kushiriki. Hii ndio mara ya kwanza kushirikisha wasichana.
Michuano
hiyo ilifunguliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Kenya, Mh Raila Odinga –
akisindikizwa na Mtendaji Mkuu wa Bharti Airtel Afrika – Manoj Kohli.
Michuano
hiyo pia itaashiria uzinduzi wa kliniki mbili za soka za kimataifa
zitakaozoendezwa na makocha kutoka klabu kubwa duniani – Arsenal na
Manchester United – zote za Uingereza.
Kwenye
uzinduzi wa michuano hiyo pia walikuwepo wawakilishi kutoka kwenye
Klabu hizo ambao ni Mkurugenzi wa Masoko kutoka Timu ya Manchester
United,Jonathan Rigby na Mkurugenzi Masoko kutoka Arsenal Angus Kinnear.
Uzinduzi wa kliniki utafanyika na wachezaji wa zamani wa Manchester
United Peter Schmeichel na Ray Parlour kutoka Arsenal.
Kwenye
mechi za ufunguzi, timu ya wasichana ya Kenya ilishushia kipigo cha
magoli 11 wenzao wa Malawi wakati kwa upande wa wavulana Malawi
ilishinda 5- dhidi ya Kenya.
No comments:
Post a Comment