HELKOPTA ZA UGANDA ZILIZOPOTEA ZAONEKANA MLIMA WA KENYA, WANAJESHI WAWILI WAFARIKI
Na Shirika la AFP
Waokoaji waligundua mabaki ya helikopta mbili za Uganda zilizokuwa zimepotea
karibu na Mlima wa Kenya siku ya Jumanne (tarehe 14 Agosti), huku
wanajeshi wawili wa Uganda wakifariki dunia na watano wakipatikana
wakiwa hai.
Rubani
wa ngazi za juu wa Jeshi la Anga la Uganda, Chris Kasaija, aliokolewa
maeneo ya Nanyuki kutoka katika mabaki ya helikopta yake.
Mabaki
ya helikopta mbili za jeshi la Uganda yaligunduliwa siku mbili baada
ya kuanguka kwenye mkoa wa mbali wa milimani wa Kenya wakati
zikielelekea Somalia kupeleka misaada.
Makala zinazohusiana
*Kikosi cha Kenya kujiunga na AMISOM wiki ijayo
*Uganda yatuma kikosi cha anga kusaidia kupambana na al-Shabaab Somalia
*Kenya kwenye tahadhari kubwa wakati vikosi vinasonga mbele kuelekea Kismayo
Mkuu
wa Jeshi la Kenya, Jenerali Julius Karangi, aliwaambia waandishi wa
habari kwamba moja kati ya helikopta hizo mbili "ilipatikana ikiwa
imeungua yote, na nyingine ikining'inia kwenye mlima". Bado watu saba
hawajulikani walipo.
Helikopta
nne ziliondoka Uganda siku ya Jumapili kwa ajili ya kuelekea mji wa
bandari wa Somalia, Kismayo, kuvisaidia vikosi vya Umoja wa Afrika
nchini Somalia katika operesheni yake ya kijeshi dhidi ya al-Shabaab.
Moja
kati ya helikopta nyengine mbili iliwasili Garissa kama ilivyopangiwa
kwa ajili ya kuwekewa mafuta, na nyingine ilitua kwa dharura kwenye
Mlima Kenya na kupiga simu ya redio kuomba msaada. Wanatimu wake saba
wako salama na imeshaokolewa.
No comments:
Post a Comment