HABARI MBALIMBALI KUTOKA SHIRIKISHO LA SOKA (TFF)
LIGI DARAJA LA KWANZA SASA TIMU 24
Ligi
Daraja la Kwanza (FDL) kuanzia msimu huu wa 2012/2013 itakuwa na timu
24 kutokana na mabadiliko ya mfumo wa mashindano yaliyofanywa na
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Kamati
ya Utendaji ya TFF ilikutana Julai 29 mwaka huu ambapo pamoja na mambo
mengine ilifanya mabadiliko ya mfumo wa mashindano ikiwemo FDL kuchezwa
kwa mtindo wa nyumbani na ugenini badala ya ule wa awali wa vituo.
Kutokana
na mabadiliko hayo, timu za FDL zitagawanywa katika makundi mawili ya
timu 12 kila moja kutokana na ukaribu wa kanda na kucheza kwa mtindo wa
nyumbani na ugenini.
Timu
ya kwanza kutoka kila kundi itapanda kucheza Ligi Kuu msimu unaofuata
wakati ya tatu itakayoungana na hizo mbili itapatikana kwa mechi za
nyumbani na ugenini kwa timu zilizoshika nafasi ya pili katika kila
kundi.
Ili
kufikisha idadi ya timu 24 kwenye FDL, Kamati ya Utendaji ya TFF kwa
kuzingatia mapendekezo ya Kamati ya Mashindano imeamua timu tatu za juu
kwenye Ligi ya Taifa kutoka vituo vyote vitatu vya ligi hiyo zimepanda
daraja.
Sasa
timu 24 za FDL ni Ashanti United (Dar es Salaam), Burkina Moro
(Morogoro), Green Warriors (Dar es Salaam), Kanembwa JKT (Kigoma),
Kurugenzi Mafinga (Iringa), Majimaji (Ruvuma), Mbeya City (Mbeya),
Mkamba Rangers (Morogoro), Mlale JKT (Ruvuma) na Morani (Manyara).
Nyingine
ni Moro United (Dar es Salaam), Mwadui (Shinyanga), Ndanda (Mtwara),
Pamba (Mwanza), Polisi (Arusha), Polisi (Dodoma), Polisi (Iringa),
Polisi (Mara), Polisi (Tabora), Rhino Rangers (Tabora), Small Kids
(Rukwa), Tessema (Dar es Salaam), Transit Camp (Dar es Salaam), Villa
Squad (Dar es Salaam) Timu
nne zitashuka daraja kurudi Ligi ya Mkoa. Timu hizo ni mbili
zilizoshika nafasi za mwisho kwa kila kundi. Timu nne zitakazopanda
kucheza FDL zitapatikana kwa mchujo utakaohusisha mabingwa wa mikoa.
Kwa
mfumo huo mpya wa mashindano, ligi za mikoa zitakazosimamiwa na
kuendeshwa na vyama vya mpira wa miguu vya mikoa zinatakiwa kuwa na timu
zisizopungua 16 na zisizozidi 20. Ligi za mikoa pia zitachezwa mwaka
mzima kwa mikondo miwili (nyumbani na ugenini).
Ligi
ya mkoa itashusha timu mbili na kupandisha nyingine mbili kutoka ligi
ya wilaya. Ligi za wilaya zitakazosimamiwa na kuendeshwa na vyama vya
mpira wa miguu vya wilaya zinatakiwa kuwa na timu zisizopungua 10 na
zisizozidi 20.
Kwa
wilaya zenye timu zaidi ya 20, chama husika cha mpira wa miguu
kitapanga utaratibu wa kuzichuja kwa mashindano ili kupata zile bora 20
zitakazocheza ligi rasmi ya wilaya.
Mabingwa
wa wilaya katika mkoa husika watacheza mechi za kuchujana (play offs)
ili kupata timu mbili zitakazopanda daraja kucheza ligi ya mkoa husika.
Kutokana
na mabadiliko hayo ya mfumo wa mashindano, sasa madaraja rasmi ya ligi
ni Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza, Ligi ya Mkoa (Ligi Daraja la Tatu)
na Ligi ya Wilaya (Ligi Daraja la Nne).TFF
inasisitiza kuwa kwa mujibu wa kalenda yake ya matukio, kipindi cha
usajili wa wachezaji kwa madaraja yote ni kimoja, na ligi zitachezwa kwa
wakati mmoja.
Usajili
wa hatua ya kwanza ni kuanzia Juni 15 hadi Agosti 10 mwaka huu wakati
kipindi cha pili cha usajili ni Agosti 21 hadi Septemba 4 mwaka huu.
Usajili wa dirisha dogo ni Novemba 15 hadi Desemba 15 mwaka huu.
Ligi
kwa madaraja yote zitaanza Septemba. Ligi Kuu itaanza Septemba Mosi
mwaka huu, Ligi Daraja la Kwanza ni Septemba 15 mwaka huu, Ligi ya Mkoa
na ile ya Wilaya zenyewe zitaanza Septemba 8 mwaka huu.
Mechi
za kufungua msimu kwa madaraja yote (Ngao ya Jamii) ambazo kwa sasa
zinakutanisha bingwa na makamu bingwa zitachezwa Agosti 25 mwaka huu
wakati michuano ya Kombe la FA itaanzia wilayani Septemba 24 mwaka huu.
BINGWA MICHUANO YA BANCABC SUPER 8 KUPATA MIL 40/-
Bingwa
wa michuano ya BancABC Super 8 inayoanza keshokutwa (Agosti 5 mwaka
huu) katika miji ya Dar es Salaam, Zanzibar, Mwanza na Arusha atapata
sh. milioni 40 wakati makamu bingwa sh. milioni 20. Pia timu mbili
zitakazoishia hatua ya nusu fainali kila moja itapata sh. milioni 15
wakati zilizobaki kila moja itapata sh. milioni 5.
Timu
zimepangwa katika makundi mawili ya A na B. Kundi A lina timu za Simba
(mabingwa wa Tanzania Bara), Jamhuri, Zimamoto na Mtende zote za
Zanzibar. Kundi ni Super Falcon (mabingwa wa Zanzibar), Azam, Mtibwa Sugar na Polisi Morogoro zote za Tanzania Bara.
Mechi
za ufunguzi keshokutwa (Agosti 5 mwaka huu) ni Simba vs Jamhuri (Dar es
Salaam), Zimamoto vs Mtende (Mwanza), Mtibwa Sugar vs Polisi Morogoro
(Arusha) na Super Falcon vs Azam (Zanzibar). Awali mashindano yalikuwa
yaanze Agosti 4 mwaka huu lakini yamesogezwa mbele kwa siku moja.
Hatua ya makundi itamalizika Agosti 12 mwaka huu. Mechi za nusu fainali na fainali zote zitachezwa Dar es Salaam.
Mdhamini
bancABC atagharamia usafiri wa ndege kwa timu zote kutoka kituo kimoja
hadi kingine, malazi na jezi. Yanga imejitokea kwenye mashindano hayo na
nafasi yake imechukuliwa na Mtibwa Sugar ambayo ilishika nafasi ya nne
kwenye Ligi Kuu ya Vodacom.
KOZI YA UONGOZI YA FIFA KUANZA AGOSTI 6
Kozi
ya Uongozi na Utawala ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu
(FIFA) itafanyika Msimbazi Center jijini Dar es Salaam kuanzia Agosti
6-11 mwaka huu ikiwa na washiriki 30.
Washiriki
wa kozi hiyo itakayonedeshwa na wakufunzi kutoka FIFA ni viongozi
kutoka TFF, Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA), vyama vya mpira wa
miguu vya mikoa, klabu za Ligi Kuu na viongozi wa mpira wa miguu wa
wanawake.Walioteuliwa
kushiriki ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa TFF, Athuman Nyamlani, Rais wa
ZFA Amani Makungu, wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF; Ahmed Mgoyi,
Blassy Kiondo, Stanley Lugenge, Khalid Abdallah, Hussein Mwamba na Eliud
Mvella.
Wengine
ni Katibu Mkuu wa ZFA, Kassim Salum, Katibu Msaidizi wa ZFA, Masoud
Attai, wenyeviti wa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa ya Kagera (Jamal
Malinzi), Dodoma (Nassoro Kipenzi) na Pascal Kihanga (Morogoro).
Makatibu
wa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa ya Mara (Mugisha Galibona),
Mtwara (Vincent Majiri), Morogoro (Hamisi Semka), Kagera (Salum Chama),
Tanga (Beatrice Mgaya) na Dodoma (Stuart Masima). Pia yumo Mwenyekiti wa
Coastal Union, Ahmed Hilal na Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement
Sanga.
Washiriki
wengine ni Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah, Mkurugenzi wa Ufundi,
Sunday Kayuni, Ofisa Habari, Boniface Wambura, Mkurugenzi wa Masoko na
Matukio, Jimmy Kabwe, Mkurugenzi wa Mashindano, Saad Kawemba, Ofisa
Sheria wa TFF, Neema Lucumay, Ofisa wa Mpira wa Miguu wa Wanawake, Grace
Buretha, Amina Karuma (Mpira wa miguu wa wanawake) na nahodha wa zamani
wa Taifa Stars, Shadrack Nsajigwa.
STARS KUIKABILI BOTSWANA AGOSTI 15
Timu
ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Agosti 15 mwaka huu itapambana na
Botswana (Zebras) katika mchezo maalumu wa Kalenda ya FIFA utakaofanyika
jijini Gaborone.
Tayari
Kocha Kim Poulsen alishatangaza kikosi cha wachezaji 21 kitakachoingia
kambini Agosti 8 mwaka huu tayari kwa mechi hiyo ya kirafiki ya kujipima
nguvu.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment