Jumatano Aug 1 2012 nilikua
nimetulia nachek bunge ghafla nikaona wabunge wanapiga meza kama kuna
shangwe flani hivi, kuja kushtuka kumbe ilikua ni kutokana na waziri wa
ofisi ya Rais aisekua na wizara maalum Profesa Mark Mwandosya kuingia
bungeni kwa mara ya kwanza baada ya kuugua kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Alisema “naona mkono wake
mwenyezi Mungu katika uponyaji wangu, ni zaidi ya mwaka tangu nimekwenda
kwa ajili ya matibabu na sijazungumza katika bunge hili tukufu, moja
kati ya mambo nilikua nasema mbona ungenirudishia hata kwa dakika tano
nije kuongea na wabunge wenzangu na mwenyezi Mungu ameliridhia ombi
langu”
Pamoja na kuwashukuru na
kuwasifu viongozi wote waliomjulia hali wa chama tawala na upinzani,
Profesa Mwandosya amesema “afya ni muhimu sana na tuendelee kupima afya
zetu wabunge, mimi miaka 45 sijawahi kuona kitanda hospitali nimekwenda
kukikuta huko Hydrebad, nilidhani ni mtu mwenye afya sana mtu wa mazoezi
kila siku asubuhi na jioni lakini kumbe mwili wa binadamu Mungu
alivyoumba ni maajabu yake yeye mwenyewe”
No comments:
Post a Comment