Ishu ya utoroshaji wa wanyama
pori ambayo juzi imefanya watumishi watatu wa maliasili kupigwa chini
iliingia kwenye page nyingine bungeni Aug 14 2012 baada ya msemaji rasmi
maliasili na utalii mchungaji Peter Msigwa kuhoji uhalali wa
kutokamatwa kwa ndege iliyobeba wanyama hao.
Amesema pamoja na kwamba Waziri
wa maliasili na utalii ametangaza kuwafukuza kazi maafisa watatu, bado
sio suluhisho la kudhibiti ujangili kwani mtandao ulioipitisha ndege ya
jeshi la Qatar ni mkubwa na unahusisha wafanyakazi wa uhamiaji, Polisi
na baadhi ya vigogo serikalini.
“serikali inahusika kwa sababu
kuna wakubwa juu yake na kuwatoa wale ni kafara, watupe taarifa ilikuja
hapa kufanya nini na ilipotoka hapa ilikwenda wapi, anadanya umma sasa
hivi eti anataka kwenda Qatar, anahitaji kwenda Qatar? – Mch Peter
Msigwa
Kwenye mistari mingine, mbunge
huyu wa Iringa mjini 92.9 amesema hajahusika kuwatetea baadhi ya
wamiliki wa vitalu vya wanyamapori kufuatia kuwa na hisa katika miradi
hiyo.
No comments:
Post a Comment