Serikali ya Malawi imepuuza
tishio la Tanzania kuhusu mzozo wa mpaka kwenye ziwa Nyasa na kusisitiza
kwamba ziwa lote ni la Malawi hivyo utafiti wa Mafuta utaendelea.
Waziri wa mambo ya ndani na
usalama wa Malawi Uladi Musa amekaririwa akiongea na radio moja na
kusema watanzania hawana mamlaka ya kuzuia utafiti wa mafuta uliokua
ukifanywa kwenye ziwa hilo, na kama shinikizo litaendelea watawasilisha
hiyo ishu kwenye mahakama ya kimataifa.
Gazeti la habari leo limeandika
kwamba waziri huyo amesema serikali ya Malawi ina ushahidi kabisa
kuthibitisha kwamba ziwa nyasa ni lao na kuna mikataba inayoonyesha,
hivyo hoja ya Tanzania haina mantiki.
No comments:
Post a Comment