Baada ya kesi yake kuendeshwa
kwa miaka sita kuhusu ishu ya uhujumu uchumi na kuisababishia serikali
hasara ya euro milioni mbili, hatimae Mahakama ya hakimu mkazi kisutu
imewaachia huru watuhumiwa ambao ni balozi wa zamani wa Tanzania nchini
Italia Profesa Costa Mahalu pamoja na ofisa utawala wa ubalozi huo Grace
Martin.
Baadhi ya waliotoa ushahidi kwa
upande wa washtakiwa ni pamoja na rais mstaafu Benjamin Mkapa kutokana
na watuhumiwa kudaiwa kuwa na baraka za ikulu wakati huo wa uongozi wa
Mkapa.
Hakimu wa Mahakama ya hakimu
mkazi Kisutu Ilvin Mgeta amesema ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na
upande wa mashtaka umeshindwa kuwatia hatiani watuhumiwa hao.
Katika kesi hiyo ambayo jumla
ya mashahidi kumi walitoa ushahidi wakiwemo watatu wa upande wa
washtakiwa na saba kwa upande wa mlalamikaji, Prof Mahalu na Grace
Martin walikua wakikabiliwa na mashtaka sita yakiwemo ya uhujumu uchumi
na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya euro milioni mbili wakati
wa ununuzi wa jengo la ubalozi wa Tanzania nchini Italia.
Baada ya hakimu kutoa kauli ya
mwisho, Watuhumiwa hao walipata nafasi ya kuzungumza ambapo Profesa
Mahalu alisema “Mungu amedhihirisha utukufu wake, kwamba Mungu siku zote
hutetea wanyonge na mimi kila wakati nilikua nikisoma Warumi 8 mstari
wa 31, Mungu akiwa na wewe hakuna atakaekua dhidi yako”
Grace Martin alisema
“Namshukuru mwenyezi Mungu kwa wema mkuu alionionyesha kwa miaka hii
yote sita, Mungu wangu ni mwaminifu sana”
No comments:
Post a Comment