Thursday, August 23, 2012
HAWA NDIO WAREMBO WAWILI WA KENYA WALIOKUBALI MWALIKO WA KUPERFORM DAR JPILI HII.
Avril na Marya ambao ni mastaa
wa hit single ya ‘Chokoza’ wamekubali mwaliko wa kulimiki stage club
Billicanas jumapili hii August 26 2012 kwenye Extreem Bash na itakua ni mara yao ya pili kuja kufanya show pamoja baada ya hiyo hit single ya ‘chokoza’.
Nafahamu kwenye vyombo vingi
vya habari stori iliyochukua nafasi kubwa sana ni pamoja na hukumu
iliyotolewa na mahakama iliyomuondoa kwenye ubunge aliekua mbunge wa
jimbo la Igunga Dokta Dalaly Peter Kafumu.
Sasa stori mpya kuhusu hiyo
hukumu imetoka kwa chama cha mapinduzi kwenyewe ambacho kimetefakari
hukumu hiyo na kimejiridhisha kufanya uamuzi wa kukata rufaa kwa sababu
haijaridhishwa.
Nape Nnauye ambae ni katibu wa
halmashauri kuu ya CCM itikadi na uenezi amesema “tutakata rufaa kupinga
uamuzi wa mahakama, hakuna kipya cha msingi ni kwamba tumeamua kukata
rufaa, hatukuridhika na hoja zilizotumiwa na jaji kuutengua ushindi wa
chama cha Mapinduzi na tunaamini kwenye rufaa tutashinda, hoja za
Mahakama ni dhaifu sana”
MWAMVITA MAKAMBA ALA SHAVU LA KUHAMIA J’BURG-SOUTH AFRICA KIKAZI...!
Mwamvita Makamba
Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Mwamvita aliandika yafuatayo;
"On the 1st of September 2012, I will officially start a new wave of my career in Johannesburg South Africa, at Vodacom Group. I have had a great time here at home, learnt a lot and grew tremendously personally and professionally.
Thanks to all of you for the support and encouragement as I went about my daily activities here. I will continue to keep in touch and keep sharing my various adventures whenever I go and get stories worth sharing with you. Remember, no matter who you are or where you come from, if you dare to dream, the world is truly your centre stage.
Love, Mwamvita"Mwamvita alipokwenda kumuaga Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ofisini kwake.Picha kwa hisani ya Ofisi ya Waziri Mkuu
HAYA NDO MABASI YAENDAYO KASI YATAKAYOTUMIKA TANZANIA
HAYA NDO MABUS YANAYOENDA KASI KULIKO DUNIANI YANAITWA METROBUS
project hii ilianza Netherland,then Turkey wakacopy,then germany na sasa hivi
Tanzanıa ndo wanatengeneza jijini Dar es salaam.
MCHAKATO WA SERENGETI FIESTA 2012 WAENDELEA KUPAMBA MOTO NDANI YA JIJI LA TANGA
Mchakato
wa Serengeti Fiesta 2012 ndani ya Tanga ukiendelea ndani ya mitaa
kadhaa ya jiji hili. Mtangazaji wa Clouds Fm Adamu Mchomvu, hapa vijana
wa kazi kutoka Clouds Fm wakiongea na wakazi wa eneo la Magaoni, Taili
Tatu Kata ya Mabawa. Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika tarehe
26.8.2012 katika uwanja wa Mkwakwani.
Mtangazaji
wa Clouds Fm Adamu Mchomvu, akiyaendeleza mastori ndani ya kitaa cha
Taili tatu eneo la Magaoni, Kata ya Mabawa, Tanga.
Mwanadada Loveness Love akiwa na Gossip Cop Tz, Sudi Brown.
...Wakionyesha umahili wao wa kunwaga.
... aha... mimi ni msela siwezi kwenda jela...
... vijana walijitahidi kuonyesha umahili wao wa kuchana michano.
... Clouds Tv nayo haikukosa.
Rasi akionyesha umahili wake wa kuimba rege.
Adamu Mchomvu akisababisha mambo.
Gossip- Cop Tz Sudi Brown akiwa katika pozi.
Mazungumzo ya mtaani yakiendelea.
Mtangazaji wa Clouds Fm Adamu Mchomvu na Mwanadada Loveness Love.
...hata jamaa alikuwa akitiririka machache ndani ya Clouds Fm/Clouds TV.
Producer wa Home record ya Tanga nae akimwaga madini.
Show Love ikiendelea.
Show love ndani ya eneo la Magaoni, Taili Tatu Kata ya Mabawa.
HAYA SASA MBUYI TWITE KASHADONDOKA YOUNG AFRICANS!
BEKI wa kimataifa wa mabingwa wa klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati ‘Kombe la Kagame’ Yanga, Mbuyi Twite amejiunga na kikosi cha timu hiyo kilichopo nchini Rwanda.Twite ambaye ameziingiza katika msigano timu za Simba na Yanga baada ya kusaini mkataba katika vilabu hivyo akianza Simba na baadaye
Yanga ambayo pia imeliwasilisha jina lake katika usajili wa wachezaji katika shirikisho la Soka Tanzania (TFF) alikuwa kwao Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kwa ajili ya kuiaga familia yake.Akizungumza kwa simu kutoka Kigali nchini Rwanda, Mjumbe wa kamati ya Utendaji ya Yanga Abdallah Binkleb alisema kwamba Twite aliwasili huko jana na leo asubuhi alifanya mazoezi na wenzake katika uwanja wa Amahoro.Alisema kama mambo yakienda vema huenda nyota huyo aliyesajiliwa kutoka APR ya huko kesho atashuka katika dimba la Amahoro akiwa ametinga uzi wa njano na kijani katika mchezo wao na Rayon utakaopigwa jioni.
Subscribe to:
Posts (Atom)